Abu Bakr – Ni Mfani Halisi wa Wema na Huruma

Wakati mmoja, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliuliza kutoka kwa Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum), “Ni nani miongoni mwenu anafunga leo?” Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu) akajibu: “Mimi Nimefunga leo.”

Nabi (sallallahu ‘alaihi wasallam) akauliza: “Ni nani miongoni mwenu aliyemtembelea mgonjwa leo? Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu) akajibu, “Mimi Nimemtembelea mgonjwa leo.

Nabi (sallallahu ‘alaihi wasallam) akauliza zaidi, “Ni nani kati yenu aliyeshiriki katika Janaazah leo?” Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu) akajibu, “Mimi Nimeshiriki katika Janaazah leo.”

Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akauliza: “Ni nani kati yenu ambaye amemlisha masikini leo?” Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu) akajibu, “Mimi Nimemlisha masikini leo.

Baada ya hapo Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema: “Mwenye sifa zote hizi bila shaka ataingia Jannah.

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …