Kumswalia Nabi wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Wakati wa Kuamka kwa ajili ya Swala ya Tahajjud.

عن سيدنا عبد الله بن مسعود قال: يضحك الله إلى رجلين رجل لقي العدو وهو على فرس من أمثل خيل أصحابه فانهزموا وثبت فإن قتل استشهد وان بقي فذلك الذي يضحك الله إليه ورجل قام في جوف الليل لا يعلم به أحد فتوضأ فأسبغ الوضوء ثم حمد الله ومجده وصلى على النبي صلى الله عليه وسلم واستفتح القرآن فذلك الذي يضحك الله إليه يقول انظروا إلى عبدى قائما لا يراه أحد غيري (عمل اليوم والليلة، الرقم: ٨٦٧، وسنده صحيح كما في القول البديع صـ ٣٧٦)

Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) amesema, “Allah subhaana wata’ala huwa anafurahishwa na watu wawili. Wa kwanza ni mtu anayekutana na adui huku akiwa amepanda farasi bora miongoni mwa marafiki zake. Marafiki zake kisha wanashindwa huku yeye akiendelea kuwa imara na anavumilia. Akiuawa basi anapata kifo cha kishahidi, na akinusurika basi anakuwa mtu ambaye Allah subhaana wata’ala ameridhika naye. Wa pili ni mtu ambaye husimama usiku (mbele ya Mwenyezi Mungu akiswali swalaah ya tahajjud) bila ya mtu yoyote kufahamu kuamka kwake kuswali. Huwa akifanya udhu kamili kisha kumsifu Mwenyezi Mungu na kumtukuza, na kumtumia salaah na salaam juu ya Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Kisha anaanza kisomo cha Qur-aan tukufu. Huyu ndiye mtu ambaye Allah subhaana wata’ala humridhia. Allah subhaana wata’ala Anasema kuhusu yeye, ‘Tazama mja Wangu ambaye amesimama (katika Swalaah) na hakuna anayemuona (akiswali) isipokuwa Mimi.

Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa Wingi

Haafidh Abu Nu’aim (rahimahullah) anaripoti kwamba Sufyaan Thauri (rahimahullah) anaeleza:

Wakati fulani nilikuwa natoka nyumbani kwangu na macho yangu yalimuangukia kijana mmoja ambaye alikuwa anasoma: اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَّعَلٰى آلِ مُحَمَّدٍ kwa kila hatua aliyochukuwa. Nikamuuliza “Je, kuna uthibitisho wowote kwa zoezi lako (au nimaoni yako tuu)?” Akauliza, “Wewe ni nani?” Nikamjibu, “Sufyaan Thauri.” Akaniuliza, “Sufyaan wa Iraq?” Nilijibu kusema ndio.

Kisha akauliza, “Je, unamtambuwa Mwenyezi Mungu?” Nlijibu kwa kusema ndio. Akauliza, “Vipi ulipata utambuzo wake?” Nikasema, “Anauchukua usiku katika mchana na kutoka mchana anauleta usiku, na humtengeneza mtoto tumboni mwa mama yake.” Alisema, “Hakika wewe hujamtambua Allah subhaana wata’ala ”

Kwa hivyo nilimuuliza, “Basi wewe umepataje kumtambua Allah subhaana wata’ala?” akajibu, “Mimi huamua kwa uthubutu kufanya jambo fulani, lakini ninaishia kuwa kutokukifanya. Ninaweka nia kufanya jambo fulani, lakini naona kwamba siwezi kulitimiza. Kupitia hili, nimegundua kuwa kuna mtu mwingine anayesimamia mambo yangu.”

Kisha nikamuuliza kuhusu usomaji wake wa salaa na salaam kwa kila hatua. Akasema, “Nilikuwa nikisafiri kwa ajili ya kuhiji na mama yangu, lakini yeye alifariki safarini. Baada ya kufa, uso wake ikawa mweusi na tumbo lake lilivimba, kwa njia ambayo niligundua kwamba alikuwa amefanya dhambi kubwa.

“Niliponyanyua mikono yangu kuelekea mbinguni kuomba dua kwa Allah subhaana wata’ala,Niliona wingu likitoka katika Tihaamah (Hijaaz) na mtu mmoja akitokea. Alipitisha mkono wake juu ya uso wa mama yangu akisababisha mwanga uonekane katika uso wa mama yangu, na akapitisha mkono wake juu ya tumbo lake na kusababisha uvimbe kuondoka.

“Nikamuuliza, ‘Wewe ni nani? umepunguza hili msiba mkubwa kutoka kwa mama yangu na mimi.’ Akajibu, ‘Mimi ni nabii wako Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam)”

“Kisha nikamwomba ushauri wowote, ambao Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akisema ‘kila ukichukuwa hatua, basi soma.

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَّعَلٰى آلِ مُحَمَّدٍ

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …