Malaika ambaye amesimama kwenye kaburi la baraka la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kufikisha salaam za ummah

عن عمار بن ياسر رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه و سلم إن الله وكل بقبري ملكا أعطاه الله أسماء الخلائق وفي رواية أسماع الخلائق  فلا يصلي علي أحد إلى يوم القيامة إلا أبلغني باسمه واسم أبيه هذا فلان بن فلان قد صلى عليك – (رواه البزار كما في الترغيب والترهيب، الرقم: 2574 ،قال الهيثمي: رواه البزار وفيه ابن الحميري واسمه عمران يأتي  الكلام عليه بعده … قال البخاري: لا يتابع على حديثه وقال صاحب الميزان : لا يعرف ونعيم بن ضمضم ضعفه بعضهم، وبقية رجاله رجال الصحيح كذا في مجمع الزوائد، الرقم:  ١٧٩٢١)

_Ammaar Bin Yaasir (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Allah subhaana wata’ala ameteua malaika kubaki karibu na kaburi langu, malaika ambaye Allah subhaana wata’ala alimpa ujuzi wa majina (na katika riwaya nyingine, uwezo wa kusikia sauti) ya viumbe vyote. kwa hivyo, hakuna mtu atakayetuma salaam juu yangu hadi siku ya qiyaamah, isipokuwa ananifikishia  na jina lake na jina la baba yake. (atasema,) huyu ni fulani na  mtoto wa fulani, ambaye ametuma salaam juu yako._

Tukio la Sayyed Ahmad Rifaa’ee (rahimahullah)

Sayyed ahmad rifaa’ee (rahimahullah) anajulikana sana kama mmoja wa wachamungu wakuu wa Uislam. katika mwaka wa 555 A.h., aliendelea kufanya hajj. baada ya hapo, alitembelea madina munawwarah, na alipokuwa amesimama mbele ya kaburi ya baraka ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), alisoma shairi ifuatayo:

في حالة البعد روحي كنت أرسلها

تقبل الأرض عني فهي نائبتي

وهذه نوبة الاشباح قد حضرت

فامدد يمينك كي تحظى بها شفتي

kutoka mbali  nilituma roho yangu kwa niaba yangu kukusalimia mahali pako pa kupumzika hapa sasa, ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) mwili wangu kukusalimu nyoosha mkono wako ili mdomo wangu ukubusu

Wakati wa kusoma shairi hizi, mkono wabaraka wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ulitoka kaburini, na mbele ya wageni wanaokadiriwa kuwa 90,000 sayyid Ahmad rifaa’ee (rahimahullah ) akaibusu. wote walipata bahati ya kuuona mkono wa baraka wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), na miongoni mwa waliokuwepo alikuwepo sheikh Abdul Qaadir Jeelani (rahimahullah).

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …