Imani kumhusu Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

4. Allah subhaana wata’ala alikuwa amembariki Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na vyeo vya juu ikilinganishwa na wengine. Kutokana na matokeo yote na manabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) ambao walikuja ulimwenguni, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa mkuu kwa kiwango na aliyependwa zaidi kwa Allah subhaana wata’ala Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alibarikiwa na Allah subhaana wata’ala na kiwango cha kuwa kiongozi wa wote wa rasul na manabii (sallallahu ‘alaihi wasallam).[1]

5. Allah subhaana wata’ala alimbariki Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa neema nyingi maalum ambazo manabii na marasul (alahis salaam) wengine hawakupewa. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema:

“Nilibarikiwa na neema sita ambazo hazikupewa na manabii wengine (sallallahu ‘alaihi wasallam); Nilibarikiwa na jawaami’ul kalim (hutuba kamili yaani: Quraan tukufu na hadeethi Mubaaraka Ambazo maana nyingi ya undani unaeleweka kwa maneno machache),  Nilisaidiwa kimungu na hofu isiyo ya kawaida ikiingia ndani ya mioyo ya makuffaar. kwangu ingawa mimi ni nipo Mbali naona kutoka umbali wa safari ya vinywa , nyanja za vita ziliruhusiwa kwangu, dunia nzima ilifanywa mahali ya mimi kuswali salaah na dunia nzima ilifanywa chanzo cha utakaso (Yaani tayammum kwa kukosekana kwa maji) kwangu, nilijulikana kama mjumbe kwa viumbe wote (mwanadamu na jini), na nilikuwa nimewekwa muhuri wa manabii wote.”[2]

6. Baraka kubwa ambazo Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokea kutoka kwa Allah subhaana wata’ala ilikuwa baraka ya mi’raaj. Mi’raaj nikuhusu safari ya miujiza ambayo Rasulullah alichukuliwa kutoka makkah mukarrama hadi baytul maqdis. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alichukuliwa katika safari hii na mwili wake katika hali ya kuamka .Baada ya kufika baytul maqdis, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliamriwa kuongoza manabii wote na marasul (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika salaah ambayo ilimaanisha kuwa alikuwa kiongozi wa manabii wote wa Allah subhaana wata’ala kutoka hapo, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipelekwa mbingu saba na kwingineko, mpaka alipobarikiwa na maono ya jannah na jahannum na heshima ya kumuona allah subhaana wata’ala na kuzungumza naye. Ilikuwa wakati wa safari hii ambapo Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokea zawadi ya salaa tano za kila siku.[3]


[1]تِلْكَ ٱلرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلٰى بَعْضٍ (سورة البفرة: ٢٥٣)

عن أبي هريرة أن النبي صلى الله عليه وسلم قال فضلت على الأنبياء بست أعطيت جوامع الكلم ونصرت بالرعب وأحلت لي الغنائم وجعلت لي الأرض طهورا ومسجدا وأرسلت إلى الخلق كافة وختم بي النبيون (صحيح مسلم، الرقم: ٥٢٣)

آمنا بذلك كله وأيقنا أن كلا من عنده وأن محمدا عبده المصطفى ونبيه المجتبى ورسوله المرتضى، خاتم الأنبياء وإمام الأتقياء وسيد المرسلين وحبيب رب العالمين (العقيدة الطحاوية صـ ٢٦)

[2] خُصَّ سيدنا رسول الله صلى الله عليه وسلم بخصائص لم يعطها الأنبياء قبله. فعن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: فضلت على الأنبياء بست: أعطيت جوامع الكلم، ونصرت بالرعب، وأحلت لي الغنائم، وجعلت لي الأرض مسجدا وطهورا، وأرسلت إلى الخلق كافة، وختم بي النبيون (رواه الترمذي، الرقم: ١٥٥٣ وقال: هذا حديث حسن صحيح).

[3] سُبْحٰنَ الَّذِىْ أَسْرٰى بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ المَسْجِدِ الحَرَامِ إِلَى المَسْجِدِ الْاَقْصَا الَّذِىْ بٰرَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ اٰيٰتِنَا ج إِنَّهُ هُوَ السَّمِيْعُ البَصِيْرُ (سورة بني إسرائل: ١)

فالإسراء وهو من المسجد الحرام إلى بيت المقدس قطعي ثبت بالكتاب والمعراج من الأرض إلى السماء مشهور ومن السماء إلى الجنة أو على العرش أو غير ذلك آحاد (شرح العقائد النسفية صـ ١٧٠)

والمعراج حق وقد أسري بالنبي صلى الله عليه وسلم وعرج بشخصه في اليقظة إلى السماء ثم إلى حيث شاء الله من العلى وأكرمه الله بما شاء وأوحى إلى عبده ما أوحى (العقيدة الطحاوية صـ ٢٨)

والمعراج لرسول الله عليه السلام فى اليقظة بشخصه إلى السماء ثم إلى ما شاء الله تعالى من العلى حق (العقائد النسفية صـ ١٦٩)

About admin

Check Also

Imani kuhusu Malaika

1. Malaika ni viumbe vya Allah subhaana wata’ala visivyo na dhambi na wameumbwa kutokana na …