Salaah na salaam kufikishwa kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kupitia Malaika

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: ليس أحد من أمة محمد يصلي على محمد أو يسلم عليه إلا بلغه يصلي عليك فلان ويسلم عليك فلان (مسند إسحاق بن راهويه، الرقم: ٩١١، ورجاله ثقات إلا أبا يحيى القتات، ففيه ضعف)

Sayyidina Ibin  Abbas (radhiyallahu ‘anhuma) mara moja aliwahi kutaja yafuatayo, “hakuna mtu kutoka kwa umma wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ambaye hutuma salaah na salaam juu ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) isipokuwa kwamba anafikishiwa kwake (kupitia malaika) na anaambiwa, “fulani na fulani amekuswalia ,na fulani na fulani ametuma salaam juu yako.”

Thawabu za kuandika (Sallallahu Alaihi Wasallam)

Hasan bin Muhammad (rahimahullah ) anasema:

niliwahi kumuona Imaam ahmad bin Hambal (rahimahullah) ndotoni mara moja. akaniambia, “laiti ungeweza kushuhudia kwa  macho yako thawabu kubwa na baraka zinazo ng’aa kabla yetu kwa wale wanaoandika salaah na salaam juu ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika vitabu vyao.” (Al-Qawlul Badee, Pg,486)

Maelezo: wakati wa kuandika jina la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), basi mtu anapaswa kuandika kwa ukamilifu (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa Kiarabu au ‘sallallahu’ alaihi wasallam ‘kwa Kiingereza. mtu hatakiwi kutosheleza na kuandika kwa kifupi kama vile ‘SAW’ au ‘PBUH’ n.k kwani hii haiendani na mahitaji ya heshima ambayo inapaswa kuonyeshwa kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam).

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …