Salaam Ya Umma Kumfikia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن أبي هريرة قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم لا تجعلوا بيوتكم قبورا ولا تجعلوا قبري عيدا وصلوا علي فإن صلاتكم تبلغني حيث كنتم (سنن أبي داود، الرقم: 2042، وإسناده جيد كما في البدر المنير 5/290)

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Msiifanye nyumba zenu iwe makaburi (Yaani jaazeni nuru nyumbani mwenu na aa’maal meema mfano salaah, kusoma quraani takatifu n.k, ili nyumba zenu zisiwe kama kaburi ambalo halina aa’maal), na msifanye kaburi langu kuwa mahali ya sikukuu, na tuma salaam kwangu, kwa hakika salaam yako inanifikia (kupitia malaika) kutoka popote ulipo.”

Kuandik ”sallallahu ‘alaihi wasallam” wakati wa kunukuu hadithi

Abul Hasan Maimooni (rahimahullah) anasema:

Nilimuona ustaadh wangu, Abu Ali (rahimahullah) katika ndoto. Niligundua kuwa kuna kitu kimeandikwa kwenye kidole chake kwa dhahabu au zafarani. Nikamuuliza, “Ewe Abu Ali, hii ni nini?” alijibu, “kila nilipokutana na jina la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) wakati nikinukuu hadithi, nilikuwa naliandika ”sallallahu ‘alaihi wasallam” (na hii ndio tuzo ya kuandika salaam).” (Al-Qawlul Badee, Pg, 487)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …