عن أنس بن مالك قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من صلى علي صلاة واحدة صلى الله عليه عشر صلوات وحطت عنه عشر خطيئات ورفعت له عشر درجات (سنن النسائي، الرقم: ١٢٩٧، وسنده حسن كما في المطالب العالية ١٣/٧٨٥)
Sayyidina Anas Binn maalik (radhiyallahu ‘anhu) Anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Alisema, “Yoyote anayenitumia salamu mara moja, Allah subhaana wata’ala Atatuma baraka kumi juu yake, dhambi zake kumi zitafutwa na daraja lake litapandishwa kwa hatua kumi.”
Mwandishi wa dalaa’ilul khairaat
Imetajwa kuhusu mwandishi wa dalaa’ilul khairaat kwamba aliwahi kufunga safari. Wakati wa safari, alihitaji maji ya kufanya wudhu. Baadaye, alikutana na kisima, lakini kwa sababu ya kutokuwa na ndoo na kamba, hakuweza kuchota maji kutoka kwenye kisima. Kwa kujali salaah yake, alikuwa na wasiwasi sana.
Wakati alikuwa katika hali hii, msichana mdogo (ambaye halikuwa bado haja baaligh) alimwona na alikuja kwake. Akamuuliza kunashida gani, naye akamueleza shida. Hapo hapo akatema mate ndani ya kisima ambacho maji yaliongezeka hadi juu ya kisima yenyewe.
Kushuhudia muujiza huu uliofanywa na msichana huyo mchanga, alishikwa na mshangao na akamuuliza msichana huyo, “ulifanyaje muujiza huu?” msichana alijibu, “hii ilikuwa kupitia baraka za salaam ambazo nimemsomea Nabii (sallallahu alaihi wasallam) “ni muujiza huu uliomsukuma kuandika kitabu dalaa’ilul khairaat.
Allaamah zardaq (rahimahullah) Anaripoti juu ya kufariki kwa mwandishi wa dalaa’ilul khairaat, harufu nzuri ya miski na kahawia iliyokuwa ikinukia kutoka kaburini. Hii ilitokana na baraka za salaam. (Fadail-e-Durood, Pg,152)