عن أبي هريرة قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من صلى علي مرة واحدة كتب الله عز وجل له بها عشر حسنات (مسند أحمد، الرقم: ٧٥٦١، ورجاله رجال الصحيح غير ربعي بن إبراهيم وهو ثقة مأمون كما في مجمع الزوائد، الرقم: ١٧٢٨٢)
Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Yoyote atakayetuma salaam juu yangu mara moja, Allah subhaana wata’alah atamwandikia fadhila kumi (katika kitabu chake cha matendo).”
Faida ya kusoma salamu elfu moja siku ya Ijumaa
Abu Abdir Rahmaan al-muqri (rahimahullah) anaripoti kuwa khallaad Bin katheer (rahimahullah) alikuwa kwenye maumivu ya kifo. Chini ya mito yake, kipande cha karatasi kilipatikana ambayo iliandikwa:
هٰذِهِ بَرَاءَةٌ مِنَ النَّارِ لِخَلَّادِ بْنِ كَثِيْرٍ
Hii ni cheti cha uhuru kutoka kwa moto wa jahannum kwa Khallaad Bin Katheer.
Watu ndipo wakauliza kutoka kwa mkewe kwa sababu ya yeye kupata bahati hii. Alijibu kwamba ilikuwa kawaida yake kusoma salamu zifuatazo mara elfu moja kila Ijumaa:
اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ
Ewe Allah subhaana wata’alah, toa salamu yako bora zaidi kwa Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) Nabii asiye jua kusoma.