Salaam itapimwa kwa kiwango cha kipimo kikamilifu.

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من سره أن يكتال بالمكيال الأوفى إذا صلى علينا أهل البيت فليقل اللهم صل على محمد النبي الأمي وأزواجه أمهات المؤمنين وذريته وأهل بيته كما صليت على آل إبراهيم إنك حميد مجيد (سنن أبي داود، الرقم: ٩٨٢، وسكت عليه هو والمنذري في مختصره، الرقم: ٩٨١)

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) anasema, “yule anayetaka salamu yake juu yangu ipimwe kwa kiwango kilicho pimwa kamili (na hivyo kupokea tuzo kamili kwa salaam) wakati akisoma salaam juu yetu, na ahlul bayt, basi anapaswa kusoma salaam ifuatayo:

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ وَأَزْوَاجِهِ أُمَّهَاتِ الْمُؤْمِنِيْنَ وَذُرِّيَّتِهِ وَأَهْلِ بَيْتِهِ كَمَا صَلَّيْتَ عَلٰى آلِ إِبْرَاهِيْمَ إِنَّكَ حَمِيْدٌ مَجِيْدٌ

Ewe Allah subhaanawata’ala! tuma salaamu kwa Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) Nabii asiye juwa kusoma, wake zake, mama wa waumini, kizazi chake na watu wa nyumba yake kama jinsi ulivyotuma salaamu kwa familia ya Ebrahim (alahis salaam), hakika wewe ndiye unastahili sifa, mwingi wa kupandisha.

kujishughulisha na salaam wakati wa majanga

Shekhe Hakeem Muhammad akhtar saheb (rahimahullah) alitaja yafuatayo:

Shekhe Ashraf Ali thaanwi (rahimahullah) alikuwa ameandaa kitaab kinaitwa “Nushrat-Teeb” kuhusu mapenzi ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kitaab kizima kinahusu upendo kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), na kupitia kusoma kitaab hiki, mtu anaweza kupima mapenzi mazito ndani ya moyo wa mwandishi wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam).

Wakati Shekhe Ashraf Ali thaanwi (rahimahullah) alikuwa akihusika katika mkusanyiko wa Nashrut-Teeb, thanabowan (mji ambao Shekhe Thaanwi (rahimahullah) aliishi) ulipatwa na pigo. Iligundulika kuwa siku ambayo Shekhe Thaanwi (rahimahullah) aliandika sehemu yoyote ya kitaab hiki, hakupata ripoti zawatu wanao kufa kuhusu pigo. Hata hivyo, siku ambayo Shekhe thaanwi (rahimahullah) hakuandika sehemu yoyote ya kitaab, ripoti za watu wengi wanaokufa zilikuwa zinasikika.

Pindi uchunguzi huu ulipomfikia Shekhe Thaanwi (rahimahullah) kupitia watu wengi, alikuwa aachi kuandika kitaab hiki kwa siku yoyote. Ilikuwa kupitia barakah za kuandika juu ya fadhila na nafasi tukufu ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) wakati huo, Allah subhaana wata’ala alisababisha kuisha kwa pigo.

Baada ya kutaja tukio hilo, shekhe Hakeem Muhammad akhtar saheb (rahimahullah) alihitimisha:
kisomo cha kumtumia salaam kwa wingi kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ni faida sana katika kuondoa misiba na majanga. Kupitia kusoma salaam moja tu, daraja la mtu linainuliwa kwa hatua kumi, amali kumi nzuri zinarikodiwa katika akaunti ya mtu, na dhambi kumi zinasamehewa. Kwa maelezo zaidi, kupitia kusoma salaam kwa wingi, mtu ajaribishe kutimiza haki za mapenzi ambazo anadaiwa kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi). (Adaabu Ishqe Rasool, Pg11)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …