Kupokea Cheti cha Uhuru kutokana na Unafiki na moto wa Jahannam

عن أنس بن مالك قال: قال رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم: من صلى علي صلاة واحدة صلى الله عليه عشرا ومن صلى علي عشرا صلى الله عليه مائة ومن صلى علي مائة كتب الله له بين عينيه براءة من النفاق وبراءة من النار وأسكنه الله يوم القيامة مع الشهداء (المعجم الصغير للطبراني، الرقم: ٨٩٩، وقال الهيثمي في مجمع الزوائد (الرقم: ١٨٢٩٨): رواه الطبراني في الصغير والأوسط وفيه إبراهيم بن سالم بن شبل الهجيمي ولم أعرفه وبقية رجاله ثقات، وقال المنذري في الترغيب والترهيب (الرقم: ٢٥٦٠): وفي إسناده إبراهيم بن سالم بن شبل الهجعي لا أعرفه بجرح ولا عدالة)

Anas (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, “yoyote atakae nitumia salaam mara moja, kwa kumlipa Allah subhaana wata’alah atamtumia salamu mara kumi (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara kumi, Allah subhaana wata’alah atamtumia salaam mara mia (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara mia, Allah subhaana wata’alah Atamwandikia (cheti) uhuru, katikati ya macho yake mawili, kutokana na unafiki, (na cheti ya) uhuru kutokana na moto wa jahannum, na Allah subhaana wata’alah ataampa heshma na faraja ya kuwa na mashahidi siku ya qiyamah.”

Harufu Nzuri kwa sababu ya kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam)

Shemeji wa shekhe Faizul Hasan Sahaaranpuri (rahimahullah) aliwahi kumwambia shaikhul hadeeth shekhe Muhammad Zakariyya kwamba baada ya kifo ya shekhe Faizul Hasan (rahimahullah), harufu nzuri ilikuwa inatoka kwenye chumba chake. Hii hali iliendelea kwa muda wa mwezi mzima baada ya kifo chake.

Pindi hii hali ilielezwa kwa shekhe Qaasim Naanotwi, alisema, “hii ni barakah ya salaam alikuwa anamtumia Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) Ndani ya maisha yake, shekhe Faizul Hasan saheb (rahimahullah) alifanya iwe tabia yake kumtumia salaam Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam), haswa usiku wa ijuma (yaani: usiku kabla wa siku ya ijuma). (Fadail-e-Durood, Pg,153)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …