Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl – Sehemu Ya Kwanza

1. Elekea qibla ukiwa unafanya ghusl. Ni vizuri kuvaa nguo kufunika sehemu za siri ukiwa unaoga.[1]

2. Oga kwenye sehemu ambayo mtu hawezi kukuona. Ni vizuri kuoga na sehemu za siri zikiwa zimefunikwa. Hata hivyo inaruhusiwa kama mtu yuko sehemu iliyofungwa (mf: bafuni) na mtu anaoga bila kufunika sehemu za siri.[2]

عن يعلى رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم رأى رجلا يغتسل بالبراز بلا إزار فصعد المنبر فحمد الله وأثنى عليه ثم قال صلى الله عليه وسلم إن الله عز وجل حيي ستير يحب الحياء والستر فإذا اغتسل أحدكم فليستتر (سنن أبي داود، الرقم: ٤٠١٢)[3]

Sayyidina Ya’laa (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba wakati mmoja, Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alimuona mtu anafanya ghusl sehemu iliyo wazi, bila vazi la chini (yaani sehemu zake za siri ziko wazi). Baadaye Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alipanda mimbar, alimshukuru Allah subhaana wata’alah na akampa utukufu wake, na baada ya hapo akasema, “kwa hakika Allah subhaana wata’alah nimkareem (yaani anawashughulikia watumishi wake kwa kiwango cha juu sana cha adabu na heshima) na amejificha (kutoka kwa macho ya watumishi wake), anapenda (watumishi wake kuwa na) hayaa na stara (pindi wakiwa wanajisaidia wenyewe au wanaoga, n.k) hivyo pindi mmoja wenu akiwa anaoga, Inabidi afiche mwili wake.”

3. Ikiwezekana tumia ndoo kuoga.[4]


[1] كذا يسن … الاستقبال (تحفة المحتاج 1/297)

[2] لا يجوز الغسل بحضرة الناس إلا مستور العورة فإن كان خاليا جاز الغسل مكشوف العورة والستر أفضل (المجموع شرح المهذب 2/157)

[3] سكت الحافظ عن هذا الحديث في الفصل الثاني من هداية الرواة (1/236) فالحديث حسن عنده

[4] حدثتني ميمونة قالت كنت أغتسل أنا ورسول الله صلى الله عليه وسلم من إناء واحد من الجنابة هذا حديث حسن صحيح (سنن الترمذي، الرقم: 62)

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …