Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl – Sehemu Ya Pili

4. Kama unafanya ghusl ndani ya shawa basi hakikisha autumii maji vibaya. Usijishughulishe na kupaka sabuni au kunyowa nywele zisizohitajika (mf: makwapani na sehemu za siri) wakati bomba la maji lipo wazi. Huu ni uharibifu mkubwa na nisababu ya kupata madhambi.[1]

5. Anza kufanya ghusl kwa kusoma tasmiyah (بسم الله الرحمن الرحيم) na kwa kutia niyya ya kufanya ghusl ili uondowe hadath akbar (yaani: kuondoa hali ya janaba).[2]

6. Osha mikono yote miwili mpaka kwenye vifundo vya mikono mara tatu.[3]

عن عائشة رضي الله عنها زوج النبي صلى الله عليه وسلم أن النبي صلى الله عليه وسلم كان إذا اغتسل من الجنابة بدأ فغسل يديه (صحيح البخاري، رقم: ٢٤٨)

Sayyidatuna Aaisha (radhiyallahu anha), mke mweshimiwa wa Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam), ameripoti kwamba pindi Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) alikuwa anafanya ghusl, alikuwa akianza na kuosha mikono yake ya barakah.

7. Osha sehemu za siri na mkono wa kushoto na ondoa uchafu wowote kwenye sehemu za siri.[4]

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال قالت ميمونة رضي الله عنها وضعت للنبي صلى الله عليه وسلم ماء للغسل فغسل يديه مرتين أو ثلاثا ثم أفرغ على شماله فغسل مذاكيره (صحيح البخاري، الرقم: ٢٥٧)

Sayyidina Ibnu Abbaas (radhiyallahu anhuma) ameripoti kwamba sayyidatuna Maaimoona (radhiyallahu anha) alisema, “nimemuekeya Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) maji ili afanye ghusl. Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) aliosha mikono yake mara mbili au tatu, na akamwagia maji kwenye mkono wa kushoto na (kwa kutumia mkono wa kushoto) aliosha sehemu zake za siri.

8. Osha uchafu wowote unaopatikana kwenye mwili wote na mkono wa kushoto.[5]


[1] اتفق أصحابنا وغيرهم على ذم الإسراف في الماء في الوضوء والغسل وقال البخاري في صحيحه كره أهل العلم الإسراف فيه والمشهور أنه مكروه كراهة تنزيه وقال البغوي والمتولي حرام (المجموع شرح المهذب 2/152)

[2] إذا أراد الرجل أن يغتسل من الجنابة فانه يسمي الله تعالى وينوي الغسل من الجنابة أو الغسل لاستباحة أمر لا يستباح الا بالغسل كقراءة القرآن والجلوس في المسجد (المجموع شرح المهذب ٢/١٤٥)

[3] إذا أراد الرجل أن يغتسل من الجنابة … ويغسل كفيه ثلاثا قبل أن يدخلهما في الاناء (المجموع شرح المهذب ٢/١٤٥)

[4] إذا أراد الرجل أن يغتسل من الجنابة … ثم يغسل ما علي فرجه من الاذى (المجموع شرح المهذب ٢/١٤٥)

[5] أما أكمل الغسل فيحصل بأمور الأول أن يغسل ما على بدنه من أذى أولا  كالمني ونحوه من القذر الطاهر وكذا النجس (روضة الطالبين ١/٢٠٠)

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 7

26. Ni adabu kwamba mtu anapotembea na mwingine amekaa, basi anayetembea aanze kutoa salamu wa …