Thawabu ya sadaqa kupitia kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam)

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال أيما رجل مسلم لم تكن عنده صدقة فليقل في دعائه اللهم صل على محمد عبدك ورسولك وصل على المؤمنين والمؤمنات والمسلمين والمسلمات فإنها زكاة وقال لا يشبع مؤمن خيرا حتى يكون منتهاه الجنة (صحيح ابن حبان، الرقم: ٩٠٣، وإسناده حسن كما في مجمع الزوائد، الرقم: ١٧٢٣١)

Abu sa’eed khudri (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, muislamu yoyote ambaye hana chochote kutoa kama sadaqa, inabidi amtumie Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) hii salaam kwenye dua yake kwa sababu ni njia ya yeye kupata thawabu ya sadaqa na itamsafishia madhambi zake.”

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ عَبْدِكَ وَرَسُوْلِكَ وَصَلِّ عَلٰى الْمُؤْمِنِيْنَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُسْلِمِيْنَ وَالْمُسْلِمَاتِ

Ewe Allah! Mtumie salaam (yaani: umwagie rehma zako) Muhammad (sallallahu alaih wasallam), mtumwa wako na mtume wako, na uwamwagie waumini na waislam, wanaume na wanawake na rehma zako.

Nabii Muhammad (sallallahu alaih wasallam) baada ya hapo akasema, “muumini anaendelea kufanya mazuri na hariziki kabisa na mazuri ambazo amezifanya mpaka (anafariki na imani na) afike jannah”.

Kupata ukaribu maaluum wa Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam)

Qaadhi Iyaadh (rahimahullah) alikuwa ni kiongozi wama muhaddith wakati wake. Alitunga kitabu kinacho itwa Al-Shifaa kuhusu haqqi za Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) na kumtumia salaam Nabii wa allah Imeripotiwa kwamba (sallallahu alaih wasallam).

Mpwa wa Qaadhi Iyaadh (rahimahullah) aliwahi kuona kwenye ndoto kama mjomba wake Qaadhi Iyaadh (rahimahullah) alikua anakaa na Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) kwenye kiti cha enzi la dhahabu. Kuona hiyo cheo la heshma na ukaribu mjomba wake anao na nabi wa allah (sallallahu alaih wasallam) aliatharika sana na akashangaa.

Pindi Qaadhi Iyaadh (rahimahullah) alikuja kujua ndoto wa mpwa wake na shangazo lake, akamwambia, “ewe mpwa! Shikana na kitabu changu, Al-shifaa, na itumie kupata makubaliko kutoka kwa Allah Tala!”

Kwa njia hii, Qaadhi Iyaadh (rahimahullah) Alimueleza mpwa wake kwamba sababu ya yeye kubarikiwa na ukaribu maaluum wa nabi wa allah (sallallahu alaih wasallam) ulikuwa ni kitabu chake, Al-shifaa, ambacho kilikuwa kimejaa na salaam za nabi wa allah (sallallahu alaih wasallam) na qissa za upendo wa nabi wa allah (sallallahu alaih wasallam). (Bustaan ul Muhaditeen, Pg, 344)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …