عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال من صلى علي عشرا صلى الله عليه مئة ومن صلى علي مئة صلى الله عليه ألفا ومن زاد صبابة وشوقا كنت له شفيعا وشهيدا يوم القيامة (أخرجه أبو موسى المديني بسند قال الشيخ مغلطاى لا بأس به، كذا في القول البديع صـ ٢٣٦)
Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) amesema “yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara kumi, Allah subhaana wata’alah atatuma salaam kwake mara mia moja, na yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara mia moja, Allah subhaana wata’alah atamtumia salaam kwake mara elfu moja, na yoyote atakaye zidisha (kunisalia mimi) kwa ajili ya upendo (kwa ajili yangu) na kwa hamu (kwa ajili ya kutafuta thawabu), nitamuombea na nitakuwa shahidi kwa ajili yake siku ya mwisho”.
Bedui Akiwa Karibu Na Kaburi La Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)
Siku moja bedui mmoja alitembelea kaburi la Nabi wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na akasema “Ewe Allah Ta’ala, Umeamrisha kuacha watumwa huru. Hapa amelala Mjumbe Wako kipenzi zaidi na huyu hapa ni mtumwa wako kwenye sehemu yake ya mwisho ya kupumzika. Nakuomba, umwokoe mtumwa huyu mnyenyekevu kutoka kwenye moto wa Jahannam.” Sauti ikaskika ikisema, “Kwa ajili yako peke yako uliomba uhuru, kwa nini si kwa niaba ya wanadamu wote? Tumekuweka huru kutoka kwa moto wa Jahannam.”
Isma’ee anaripoti:
Siku moja bedui mmoja alisimama mbele ya kaburi la Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akisema, “Ewe Allah Ta’ala, huyu hapa amelala ni kipenzi chako. Mimi ni mja wako na Shetani ni adui wako. Ukinisamehe, kipenzi chako hapa ataridhika, mtumwa wako atafanikiwa na moyo wa adui wako hautafurahishwa. Ewe Mola wangu, usiponisamehe, moyo wa kipenzi chako utahuzunika, adui yako atafurahi sana na mja Wako huyu hatofanikiwa.
Ewe Allah Ta’ala, ni desturi miongoni mwa Waarabu kwamba kila anapofariki mtawala mkubwa miongoni mwao walikuwa wakiwaacha huru watumwa pembeni ya kaburi lake Sallallahu ‘alaihi wasallam .Ewe Allah Ta’ala, huyu hapa amelala ni mkuu miongoni mwa viongozi na watawala wote, na hapa nimesimama kama mtumwa Wako. Ewe Mwenyezi Mungu, niepushe na moto wa Jahannamu.”
Isma’ee anasema zaidi, “Niliposikia dua ya bedui huyu, nilimwambia, ‘Ewe Mwarabu, kwa dua hiyo ulioiomba na kwa namna ulioiomba, hakika Mwenyezi Mungu atakusamehe madhambi zako.