Kupata Thawabu Sabini

عن عبد الرحمن بن مريح الخولاني قال سمعت أبا قيس مولى عمرو بن العاصي يقول: سمعت عبد الله بن عمرو يقول: من صلى على رسول الله صلى الله عليه وسلم صلاة صلى الله عليه وملائكته سبعين صلاة فليقل عبد من ذلك أو ليكثر (مسند أحمد، الرقم: ٦٦٠٥، وإسناده حسن وحكمه الرفع إذ لا مجال للإجتهاد فيه كما في القول البديع صـ ٢٣٧)

Abdullah Bin Amr Bin Aas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti, “mtu yoyote atakaye mswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) mara moja, Allah subhaana wata’alah na malaika wake watamtumia rehema na baraka sabini juu yake kwa kumrudishia salaam yake ile ile moja. Baada ya hapo mtu yoyote atakae taka kuzidisha salaam zake azidishe, na yoyote atakae taka kupunguza hapunguze (yaani kama anataka kupata thawabu nyingi, basi azidishe salaam zake).

Ayyoob Sakhtiyaani (rahimahullah) katika Madinah Tayyibah

Abdullah bin Mubaarak (rahimahullah) anasema:

Nilimsikia Imaam Abu Hanifah akisema: “Wakati Ayyoob Sakhtiyaani (rahimahullah) alipokuwa Madinah Tayyibah, mimi pia nilikuwepo na nilimtazama kuona jinsi atakavyowasilisha Salaam kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Nilimwona akilitazama kaburi huku mgongo wake ukielekea kibla. Alikuwa amesimama pale bila kusema neno lolote. Badala yake, alilia tu na kulia.”

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …