Upendo wa Anas bin Nadhr (radhiyallahu ‘anhu) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na kuwa kwake shahidi katika vita vya Uhud

Wakati Waislamu walipokuwa wanazidiwa katika vita vya Uhud, habari za uongo zilianza kuenea kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ameuwawa. Hii habari zilisababisha wengi wa Maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) kukata tamaa na kupoteza moyo.

Anas bin Nadhr (radhiyallahu ‘anhu) alitokea kumuona Umar (radhiyallahu ‘anhu) na Talhah (radhiyallahu ‘anhu) pamoja na kundi la Maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) katika hali ya huzuni na kukata tamaa kabisa. Akawaambia, “Kwa nini nawaoneni ninyi nyote hivyo kama wenye kukata tamaa na wenye huzuni?” Wakajibu, “ameuwawa.”

Anas (radhiyallahu ‘anhu) akasema, “Basi ni nani anapenda kuishi baada ya yeye kufa? Njooni, twende mbele na panga zetu na tuungane na mpenzi wetu, Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)!” Muda aukupita Baada ya kutamka haya maneno yeye kujitumbukiza katika mistari ya maadui na kupigana kwa ujasiri mpaka akauawa kishahidi.

Anas (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa na mapenzi ya hali ya juu sana kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) mpaka hakuona maisha haya kuwa na thamani ya kuishi bila yeye. (Dalail un Nubuwah, 3/245)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …