Ansaari anabomoa jengo mpaka chini

Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) wakati fulani alikuwa akipitia barabara ya Madinah Munawwarah alipoona jengo likubwa. Akauliza kutoka kwa Swahaabah, “Ni nini hiki?” Wakamjulisha kwamba lilikuwa ni jengo jipya lililojengwa na Ansaari mmoja. Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akakaa kimya.

Wakati mwingine, Ansaari yule aliyojenga nyumba hiyo alikuja kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na kumsalimia kwa salamu. Basi Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) aligeuza uso wake, mbali yeye alirudia tena lakini hakujibu. Sahaabi huyu alikuwa na wasiwasi sana kwa ajili ya Rasulullah akujibu salaam yake.

Alipouliza kutoka kwa Maswahabah, walimfahamisha kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alipita karibu na jengo lipya alilokuwa amelijenga na kuiulizia. Hapo hapo akaenda na kulibomoa hilo jengo lipya chini, na hata hakumjulisha Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kuhusu kitendo chake.

Muda fulani baadaye, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alitokea kupita njia hiyo tena. Aliuliza, “Liko wapi lile jengo kubwa ambalo nakumbuka kuliona mara ya mwisho tulipopita hapa?” maswahaabah walimjulisha kama yule answaari alilibomoa mpaka chini, kwa vile alihisi kuwa hiyo ndiyo sababu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kuchukizwa. Wakati huo, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Alisema, “Kila muundo (ambao umejengwa bila hitaji la kweli) utakuwa mzigo kwa mtu, isipokuwa ule muundo ambao ni muhimu sana.”

Kitendo cha huyu Sahaabi ulionyesha upendo wa kweli na kujitolea. Na Maswahaabah hawakuweza kuvumilia kukasirika kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), na mara tu walipohisi kuchukizwa kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kupitia kitendo chochote kile, mara moja waliacha kitendo hicho kwa gharama yoyote ile. (Sunan Abi Dawood, #5237)

About admin

Check Also

Uhuru wa Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) na hamu ya Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) kwa Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) kuwa huru

Wakati mmoja, wakati akizungumza kuhusu Bilaal (Radhiyallahu 'Anhu), Sa'eed bin Musayyib (Rahimahullah) alisema:

Tamaa ya kuwa muisilamu ilikuwa kubwa sana moyoni mwa Bilal (Radi Allahu 'Anhu). Alikuwa akiwekwa chini na kuteswa katika mikono ya makafiri. Wakati wowote makafiri wangejaribu kumlazimisha kuachana na Uislamu, angekataa kwa nguvu na kutangaza waziwazi "Allah Allah" (yaani Allah Ta'ala ndiye mungu pekee anayestahili kuabudiwa).

Rasulullah (Sallallahu 'Alaihi Wasallam) kisha alikutana na Abu Bakr (Radhiyallahu' Anhu) na alionyesha hamu yake akisema, "Ikiwa tu tungekuwa na mali ambayo tunaweza kumnunua Bilaal (na kumwachisha huru)!" Baada ya hapo, Abu Bakr (Radhiyallahu 'Anhu) alimkaribia 'Abbaas (Radhiyallahu' Anhu) akamwambia, "Nenda umnunue Bilaal kwa niaba yangu."