عن عبد الرحمن بن مريح الخولاني قال سمعت أبا قيس مولى عمرو بن العاصي يقول: سمعت عبد الله بن عمرو يقول: من صلى على رسول الله صلى الله عليه وسلم صلاة صلى الله عليه وملائكته سبعين صلاة فليقل عبد من ذلك أو ليكثر (مسند أحمد، الرقم: ٦٦٠٥، وإسناده حسن وحكمه الرفع إذ لا مجال للإجتهاد فيه كما في القول البديع صـ ٢٣٧)
Abdullah Bin Amr Bin Aas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti, “mtu yoyote atakaye mswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) mara moja, Allah subhaana wata’alah na malaika wake watamtumia rehema na baraka sabini juu yake kwa kumrudishia salaam yake ile ile moja. Baada ya hapo mtu yoyote atakae taka kuzidisha salaam zake azidishe, na yoyote atakae taka kupunguza hapunguze (yaani kama anataka kupata thawabu nyingi, basi azidishe salaam zake).
Kuacha Madhambi kupitia Dua ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)
Ja’far As-Saa’igh (rahimahullah) Anaeleza:
Miongoni mwa majirani wa Imaam Ahmad bin Hambal (rahimahullah), kulikuwa na mtu ambaye alikuwa akiishi maisha ya madhambi na maovu. Siku moja, alihudhuria kikao cha Imaam Ahmad (rahimahullah) Alipoingia kwenye kikao cha Imaam Ahmad (rahimahullah), alimsalimia Imaam kwa salaam. Ingawa Imaam Ahmad (rahimahullah) alijibu salamu yake, mtu huyo alitambua kwamba Imaam alikuwa ameonyesha kutokumpendelea.
Alimwambia Imaam Ahmad (rahimahullah) akisema, “Ewe Abu Abdillah, naona kwamba unajisikia vibaya na kuja kwangu ( kuona kama uso wa imaam haukufurahi ilikuwa ni kwa sababu ya madhambi aliohusika nayo, akasema,) ningependa kukufahamisha kwamba nimeacha maisha yangu ya madhambi na nimeamua kuishi maisha ya utii na ya unyenyekevu.”
Akaeleza zaidi kwa Imaam Ahmad bin Hambal (rahimahullah), “Jana usiku, niliota ndoto ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam). Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akanijia na kuniuliza, ‘Kwa nini hautaki nikuombee dua kwa ajili yako?’. Nikajibu, ‘Ewe mjumbe Wa Allah Ta’ala kwa sababu ya madhambi yangu kupindukia na kuishi maisha ya kuvunja amri za Allah Ta’ala, naona haya sana kuja mbele yako.” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akasema: “Usijali, hata kama unaona haya, simama na mimi, nitaomba dua kwa Allah Ta’ala kwa niaba yako.
Kisha akasema, “Nilisimama na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na akaniombea dua. Mara nilipoamka, nilikuta kwamba Allah Ta’ala Ameweka chuki ya asili na chuki ndani ya moyo wangu kwa madhambi yote nilizohusika nazo.”