Namna Ya Kujisafisha Kutoka Kwenye Madhambi

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال صلوا علي فإنها زكاة لكم واسألوا الله لي الوسيلة فإنها درجة في أعلى الجنة لا ينالها إلا رجل وأرجو أن أكون أنا هو (مسند أحمد، الرقم: 8770، وفي مجمع الزوائد (الرقم: 1877): رواه البزار وفيه داود بن علبة ضعفه ابن معين والنسائي وغيرهما ووثقه ابن نمير وقال موسى بن داود الضبي: حدثنا داود بن علبة وأثنى عليه خيرا وقال ابن عدي: هو في جملة الضعفاء ممن يكتب حديثه)

Abuu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema, “nisalieni kwa hakika ni njia ya usafishaji wenu. Muulize Allah subhaana wata’alah anijalie daraja la “waswila” ambayo ni daraja la juu la peponi limehifadhiwa kwa mtu mmoja tu, na ninamatumaini yangu kwamba mimi ni yule ambaye amebarikiwa na hii heshima na daraja.

Heshima ya Imaam Maalik (rahimahullah)

Imaam Maalik (rahimahullah) alikuwa na mapenzi makubwa kwa ardhi ya Madinah Munawwarah. Upendo huu ulikuwa kwa sababu ya mapenzi aliyokuwa nayo kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam).

Allaamah Ibnu Khallikaan (rahimahullah) anaandika:

Imaam Maalik (rahimahullah) hakuwahi kupanda usafiri wowote katika mji uliobarikiwa wa Madina Munawwarah. Hata wakati alipokuwa mzee na alidhoofika sana, alipendelea kutembea kuliko kusafirishwa na usafiri. Imaam Maalik (rahimahullah) alipoulizwa sababu, alitaja, “Ninajihisi vigumu sana kupanda usafiri katika mji wa Mubaarak wa Madinah Munawwarah, ambapo Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amezikwa chini ya ardhi.” (Wafayatul Aayaan, 4/136)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …