Wakati Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokaribia kufariki, mkewe alianza kusema, “Ah, huzuni iliyoje! Unaondoka katika ulimwengu huu!” Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu: “Inapendeza nani furaha iliyoje kwamba kesho tutakutana na marafiki zetu, tutakutana na Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na maswahaba zake.
Soma Zaidi »Maswahaba wakijitolea kwa ajili ya Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam)
Nyumba ya Faatimah (radhiyallahu ‘anha) ilikuwa mbali na nyumba ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) siku moja alimwambia: “Ni matamanio yangu kwamba uishi karibu nami.” Faatimah (radhiyallahu ‘anha) akajibu, “Nyumba ya Haarithah iko karibu na nyumba yako. Ukimwomba abadilishe nyumba yake na yangu, atakubali kwa furaha.” Rasulullah …
Soma Zaidi »Hakuna nafasi katika Uislamu kwa wale wanaowatukana Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum)
Wakati mmoja, mtu mmoja alikuja kwa Zainul ‘Aabideen, ‘Ali bin Husein (rahimahullah), na kumuuliza: “Ewe mjukuu wa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam)! Nini maoni yako kuhusu ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu)?” Kuona chuki ya mtu huyo kwa ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu), Zainul ‘Aabideen (Rahimahullah) akamueleza kwamba kwa ujumla, kuna makundi matatu ya …
Soma Zaidi »Ushujaa wa Ali (Radhiyallahu ‘anhu) katika Uhud
Wakati wa vita vya Uhud, Maswahabah (radhiya Allaahu ‘anhum) walishambuliwa na makafiri na wengi kuuawa. Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alizungukwa na maadui na alipata majeraha kadhaa. Wakati huo, uvumi ulianza kuenea kwamba Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) ameuawa. Kusikia uvumi huu wa uongo, wengi wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walipoteza utulivu …
Soma Zaidi »Talhah (radhiyallahu ‘anhu) katika Vita vya Uhud.
Zubair bin Awwaam (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba katika tukio la Uhud, Rasulullah (sallallaahu ‘alaihi wasallam) alikuwa amevaa silaha mbili. Wakati wa vita, Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alikusudia kupanda juu ya jabali lakini kutokana na uzito wa zile silaha mbili, hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo alimwomba Talhah (radhiyallahu ‘anhu) kukaa chini …
Soma Zaidi »Mapenzi Makubwa ya Maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)
Siku moja, mtu mmoja alikuja kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na akasema: “Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) mapenzi yangu kwako ni kwamba ninapokufikiria wewe huzidiwa na mapenzi yako, kiasi kwamba sipati kuridhika mpaka nikuone. Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), mawazo yananipitia moyoni mwangu kwamba ikiwa Allah ta’ala atanijaalia Pepo, itakuwa …
Soma Zaidi »Mapenzi ya swahaba mmoja kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)
Swahaba mmoja siku moja alikuja kwa Nabii wa Allah sallallahu alaihi wasallam na kumuuliza, “Ewe! Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ni lini siku ya Qiyaamah?” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Umefanya maandalizi gani? kwa siku hiyo?” huyu swahaba akasema, “Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), sidai kuwa nina Swalaah nyingi, saumu na …
Soma Zaidi »Mapenzi ya Zaid bin Dathinah (radhiyallahu ‘anhu) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)
Makafiri walipokaribia kumuuwa sahabi mkubwa, Zaid bin Dathinah (radhiyallahu ‘anhu), wakamuuliza, “Je, ungekuwa na furaha zaidi kama Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) angekuwa katika nafasi yako na ukaachwa huru kuwa pamoja na familia yako?” Jibu lake la papo kwa papo lilikuwa, “Wallahi, siwezi hata kustahimili kuwa nimekaa kwa raha na familia …
Soma Zaidi »Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) anapoteza Meno Yake
Wakati wa vita vya Uhud, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa ameumizwa vibaya sana na adui na vipande viwili vya kofia yake vikapenya kwenye uso wake wa mubarak. Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) na Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) mara moja wakakimbia na kumsaidia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) …
Soma Zaidi »Wasiwasi wa Mwanamke wa Answaari Kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)
Katika vita vya Uhud, Waislamu walipata hasara kubwa na idadi kubwa kabisa yao waliuawa. Taarifa nzito zilipofika Madinah Munawwarah, wanawake hao walitoka nje ya nyumba zao wakiwa na shauku ya kutaka kujua undani wa vita hivyo. Alipouona umati mkubwa wa watu wamekusanyika mahali fulani, mwanamke mmoja waki Answaar aliuliza kwa …
Soma Zaidi »
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu