Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) anaeleza kuhusu safari ya Hijrah pamoja na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam).
Tulisafiri kwa haraka mchana na usiku mzima hadi joto la jioni likawa kali. Basi nilikuta barabara ni tupu na hakuna mtu anayetembea juu yake. Nilitazama mbele ili kuona kama ningeweza kupata kivuli chochote ili tujikinge humo. Kisha nikaona jiwe kubwa ambalo chini yake kulikuwa na kivuli ambacho tungeweza kujikinga na joto.
Tukasimama kando ya jabali (kutulia kwenye kivuli chake), na nikatumia mikono yangu kuifanya ardhi kuwa tambarare ili Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alale na kupumzika. Kisha nikatandaza ngozi chini na kumwambia: “Pumzika, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (Sallallahu ‘alaihi wasallam), nami nitachunga eneo lililo karibu nawe.”
Mara moja Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alilala chini ili kupumzika, nilikwenda kuangalia kama ningeweza kumwona mtu yoyote ambaye alikuwa akitutafuta. Kisha nikamwona mfugaji aliye kuwa mtumwa akija kwenye mwamba ili naye apumzike kivulini, tulipokuwa tunapumzika.
Nikamuuliza mmiliki wake ni nani, akataja mtu wa Makka ambaye nilimjua. (Kwa vile ilikuwa ni desturi iliyoenea wakati huo kwamba watu wangewaruhusu wasafiri na kunufaika na maziwa kutoka katika wanyama zao, Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) alimwomba mfugaji baadhi ya maziwa.)
Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) anasema : “Je kuna mbuzi yoyote ana maziwa?”
Mchungaji: “Ndiyo.”
Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu): “Je, utanikamulia?”
Alikubali, na kunikamulia maziwa ya mbuzi mmoja na kuyamimina ndani chombo changu. Niliongeza maji kwenye maziwa ili kupoza maziwa ya moto. Kisha nikachukua maziwa kumkabidhi Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Wakati nilimsogelea Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), nilimkuta macho. Nikasema, “Kunywa haya maziwa, Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam ”.Kumuona Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kufurahiya maziwa kulileta furaha nyingi kwa moyo wangu.”
Kuangalia tukio hili, tunaona mapenzi makubwa aliyokuwa nayo Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam), kwamba kumuona Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akinywa maziwa kulileta furaha kubwa moyoni mwake alafu hakuwa yeye aliyekuwa akinywa maziwa.
Hii inaweza kufananishwa na upendo wa mama kwa mtoto wake anapomwona mtoto akila chakula – maono yenyewe huleta furaha moyoni mwake.