Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) Akimtetea Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)

Katika tukio moja, wakati Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akiwa akiswali pembeni ya Ka’bah Sharifu, Uqbah bin Abi Mu’ait, mmoja wa viongozi waovu sana wa Maquraish, alimwendea kwa nia mbaya ya kumdhuru

Alipokuja kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), Uqbah alimvua kitamba chake, akaiweka shingoni mwake na akaanza kumnyonga nayo bila huruma.

Pindi tu Abu Bakr Siddeeq (radhiya allaahu ‘anhu) alipopata habari hii, alikimbia kwenye eneo la tukio ili kumtetea na kumlinda Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam). Kufika tu mara moja akamshika Uqbah kwenye bega na kumsukuma mbali na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam).

Abu Bakr Siddeeq (radhiya allaahu ‘anhu) kisha akamkemea Uqbah kwa maneno yafuatayo:

أَتَقْتُلُونَ رَجُلًا أَن يَقُولَ رَبِّيَ اللَّهُ وَقَدْ جَاءَكُم بِالْبَيِّنَاتِ مِن رَّبِّكُمْ

Je! Unakusudia kumuua mtu kwa sababu tu anatangaza kwamba Mola wangu ni Allah Ta’ala; wakati Amekuleteeni Ishara zilizo wazi kutoka kwa Mola wenu.

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …