Ulinzi Ndani Ya Kaburi

Zaidi ya hayo, imeripotiwa kwamba mtu ambaye ameshikamana na Qur-aan Tukufu anapofariki, kabla ya kuzikwa, wakati familia yake bado inashughulika na ibada ya mazishi yake, Qur-aan Tukufu humjia ikiwa na sura nzuri na kusimama kwenye upande wa kichwa chake, kumlinda na kumfariji mpaka avikwe na sanda. Kisha Quraan Tukufu itaingia kwenye sanda yake na kutulia kifuani mwake.

Atakapowekwa kaburini, na udongo ukawekwa juu yake, na marafiki zake wote wakaondoka, basi Malaika Munkar na Nakir watakuja kwake na kumkalisha kwenye kaburi lake. Qur’an Tukufu kisha itakuja baina yake na hawo Malaika.

Malaika watazungumza na Qur-aan Tukufu wakisema: “Ondoka mbali ili tumhoji.” Lakini, Qur-aan Tukufu itajibu, “Siondoki kamwe! Naapa kwa Mola wa Al-Ka’bah, alikuwa mtu wangu wa karibu na alikuwa rafiki yangu duniani! Kwa hiyo, sitamuacha kamwe katika hali yoyote! Ukiwa umeamrishwa kutekeleza kazi yoyote (yaani kumhoji), basi unaweza kufanya hivyo, lakini niache nibaki naye hapa, kwa sababu sitamuacha mpaka Nimuingize katika Jannah.[1]


[1] ورواه ابن أبي الدنيا وغيره عن عبادة بن الصامت موقوفا عليه ولعله أشبه كذا في الترغيب والترهيب للمنذري 1/ 245

About admin

Check Also

Fadhila za Jumu’ah

Kusamehewa Madhambi Kwa Kuswali Jumu’ah Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu …