Baada ya baba yake Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) kusilimu, Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alizungumza na Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akisema:
“Nakula kiapo kwa Yule aliye kuusieni haki! Ingawa nina furaha sana kuwa baba yangu amesilimu, furaha ambayo ningeipata kama mjomba wako, Abu Taalib, angesilimu, ingekuwa kubwa zaidi kuliko furaha ninayoipata sasa. Sababu ni kwamba kama mjomba wako, Abu Taalib angesilimu, hii ingeleta furaha kubwa kwako (kuliko furaha unayoipata juu ya Uislamu wa baba yangu).
Kusikia hivyo, Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alifurahishwa sana na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) na akashuhudia mapenzi yake ya kweli kwa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam). Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema: “Hakika umesema kweli.