Salaam Kwa Nabii ﷺ

Salaa na Salaam Maalum juu ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن أبي هريرة عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: من قال اللهم صل على محمد وعلى آل محمد كما صليت على إبراهيم وآل إبراهيم وبارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم وآل إبراهيم وترحم على محمد وعلى آل محمد كما ترحمت على إبراهيم وآل إبراهيم شهدت …

Soma Zaidi »

Salaa na Salaam Ma’luum ya Ibn Abbas (radhiyallahu ‘anhuma)

عن ابن عباس أنه كان يقول: اللهم تقبل شفاعة محمد الكبرى وارفع درجته العليا وآته سؤله في الآخرة والأولى كما آتيت إبراهيم وموسى (مصنف عبد الرزاق، الرقم: 3104، وإسناده جيد قوي صحيح كما في القول البديع صـ 122) Ibn Abbas (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba alipokuwa akimtumia salaa na salaam juu …

Soma Zaidi »

Salaa na Salaam Maalum ya Ibnu Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu)

Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) Anaeleza, “Unapomswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), basi mswalie kwa adabu bora zaidi (yaani kwa kujitolea, umakini, upendo na heshima), kwa hakika wewe hujui ya kwamba huenda hio salaa na salaam zenu zitahudhurishwa mbele yake. Wanafunzi wa Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) waliuliza, “Tufundishe jinsi ya kutuma salaa na Salaam juu ya Rasulullah sallallahu alaihi wasallam ” Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Soma yafuatayo:

Soma Zaidi »

Salaa na Salaam ya Ibrahim (‘alahi salaam)

Abdur Rahmaan bin Abi Laila (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti:

Ka’b bin Ujrah (radhiyallahu ‘anhu) aliwahi kukutana nami na kuniuliza, “Je! nikupe zawadi niliyoipata kutoka kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)? Nilijibu, “Ndiyo, kwa kweli tafadhali nipe hiyo zawadi.” Alisema, "Wakati mmoja, tulimuuliza Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), ‘Ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam), ni Namna gani kukutumia wewe na familia yako salaa na salaam, hakika Allah ta'ala ametufundisha (kupitia kwako) jinsi ya kukutumia salaa na salamu?’” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Sema.

Soma Zaidi »

Kumswalia Nabii wa Allah sallallahu alaihi wasallam katika Maeneo ambayo Watu wameghafilika.

Abu Waa’il (rahimahullah) anaeleza, “Sijawahi kumuona Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) akihudhuria mkusanyiko au mwaliko wowote, isipokuwa tu kwamba angemhimidi na kumtukuza Allah subhaana wata'ala na kumtumia salaa na salaam juu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Kama ingemlazimu kwenda sokoni, ambako alikuta watu wameghafilika na kumkumbuka Allah ta'ala, basi angemhimidi Allah ta'ala Na kumswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) katika sehemu hizo.”

Soma Zaidi »

Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) kabla ya Kufanya Dua

Fadhaalah bin Ubaid (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba katika tukio moja, pindi Rasulullah sallallahu alaihi wasallam alikuwa amekaa (msikitini), mtu fulani aliingia na kuswali. Baada ya kuswali, mtu huyo aliomba dua akisema, “Ewe Allah subhaana wata'ala! Nisamehe na unimiminie rehema zako!” kumtazama namna mtu huyu alivyoomba dua, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamwambia: “Umeharakisha (kumwomba Allah ta'ala haja yako), Ewe Mtu aliye swali! Baada ya kuswali, unapokaa kufanya dua, anza kwa kumhimidi Allah (subhaana wata'ala) kwa vile anastahiki kusifiwa. Baada ya hapo nitumie mimi salaa na salaam, kisha mletee Allah ta'ala haja yako.” Baada ya hapo, mwingine mtu aliyeswali. Baada ya kuswali, alimhimidi Allah (subhaana wata'ala), akamtumia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) salaa na salaam (na kisha akaanza kuomba). Kumwangalia mtu huyu (na yeye akishikamana na adabu za dua), Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamwambia, “Ewe mtu aliye swali! Omba dua, kwa sababu dua yako itakubaliwa!”

Soma Zaidi »

Kumswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kabla ya kusoma Dua

Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) amesema “Wakati wowote mtu kati yenu akikusudia kumwomba Allah (subhaana wata'ala), Basi aanze dua yake kwa kumhimidi na kumtakasa Allah (subhaana wata'ala) kwa sifa zinazostahiki Utukufu na heshima yake. Kisha amtumie salaa na salaam juu ya Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na baada ya hapo aombe dua, Kwa sababu (kupitia kufuata njia hii ya kuomba dua) kuna uwezekano mkubwa kwamba atakuwa amefanikiwa (katika dua yake kujibiwa)."

Soma Zaidi »