Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Kwenye Mkusanyiko

عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ما من عبدين متحابين في الله يستقبل أحدهما صاحبه فيصافحه ويصليان على النبي صلى الله عليه وسلم إلا لم يفترقا حتى تغفر ذنوبهما ما تقدم منهما وما تأخر (مسند أبي يعلى الموصلي، الرقم: 2960، وفيه درست بن حمزة وهو ضعيف كما في مجمع الزوائد، الرقم: 17987)

Anas bin Maalik (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Pindi Waislamu wawili wanaopendana (kwa ajili ya Allah Ta‘ala) wakikutana na wakamtumia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Salaa na salaam basi kabla hawaja aachana husamehewa madhambi zijazo na zilizopita (madhambi madogo madogo).”

Talha (radhiyallahu ‘anhu) katika Vita vya Uhud.

Zubair bin Awwaam (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alivaa suti mbili za kivita kwenye mwili wake katika vita vya Uhud.

Wakati wa vita, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikusudia kupanda mwamba, lakini hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo alimuomba Talhah (radhiyallahu ‘anhu) kukaa, na kwa usaidizi wake, alipanda huo mwamba. Zubair (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba alimsikia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akisema, “Imekuwa ni waajib kwa Talhah (yaani Jannah au uombezi wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ni waajib kwa Talha).”

Katika vita vya Uhud, Talhah (radhiyallahu ‘anhu) alifuatana na kumlinda Rasulullah kwa ushujaa. Wakati wowote Maswahaba walipojadili vita vya Uhud, walikuwa wakisema kwamba siku hii ni ya Talhah (radhiyallahu ‘anhu) Talhah (radhiyallahu ‘anhu) alimkinga Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na mwili wake. Alipata majeraha na madonda zaidi ya thamanini mwilini mwake, lakini hakuondoka na kuacha upande wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), ingawa mkono wake ulikuwa umepooza. (Saheeh Bukhari, 3724)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …