عن أنس رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: إذا نسيتم شيئا فصلوا علي تذكروه إن شاء الله تعالى (أخرجه أبو موسى المديني بسند ضعيف كما في القول البديع صـ 448)
Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, “ukiwa umesahau kitu, basi nitumie salaa na salaam juu yangu, utakikumbuka kama Allah subhaana wata’ala akipenda.
Upendo wa Anas bin Nadhr (radhiyallahu ‘anhu) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na kuwa kwake shahidi katika vita vya Uhud
Wakati Waislamu walipokuwa wanazidiwa katika vita vya Uhud, habari za uongo zilianza kuenea kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ameuwawa. Hii habari zilisababisha wengi wa Maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) kukata tamaa na kupoteza moyo.
Anas bin Nadhr (radhiyallahu ‘anhu) alitokea kumuona Umar (radhiyallahu ‘anhu) na Talhah (radhiyallahu ‘anhu) pamoja na kundi la Maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) katika hali ya huzuni na kukata tamaa kabisa. Akawaambia, “Kwa nini nawaoneni ninyi nyote hivyo kama wenye kukata tamaa na wenye huzuni?” Wakajibu, “ameuwawa.”
Anas (radhiyallahu ‘anhu) akasema, “Basi ni nani anapenda kuishi baada ya yeye kufa? Njooni, twende mbele na panga zetu na tuungane na mpenzi wetu, Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)!” Muda aukupita Baada ya kutamka haya maneno yeye kujitumbukiza katika mistari ya maadui na kupigana kwa ujasiri mpaka akauawa kishahidi.
Anas (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa na mapenzi ya hali ya juu sana kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) mpaka hakuona maisha haya kuwa na thamani ya kuishi bila yeye. (Dalail un Nubuwah, 3/245)