Sunna za Msikiti

25. Usipasue vifundo vyako ukiwa msikitini. Vile vile, usiunganishe vidole vyako ukiwa umeketi msikitini.

Mtumwa aliyeachiliwa huru wa Sayyidina Abu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) anasema, “Siku moja, nikiwa na Abu Sa’eedd (radhiyallahu ‘anhu) na yeye akiwa pamoja na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), tuliingia msikitini na tukamuona mtu mmoja ameketi katikati ya musjid. Mtu huyu alikuwa amekaa kitako kwa jinsi magoti yake yalivyoinuliwa, na mikono yake ikiwa imezunguka magoti yake, na vidole vya mikono yake yote miwili vimeunganishwa. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliimpa ishara mtu huyu (kuvuta mazingatio yake), lakini mtu huyo hakuona ishara ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam). Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hivyo akageuka kumelekea Abu Sa’eed (radhiyallahu ‘anhu) na akasema, ‘Mmoja wenu atakapokuwa msikitini, basi asiunganishe vidole vyake, kwani kuunganisha vidole vyake ni kutoka kwa Shetani. Kwa muda utabakia msikitini mkingojea Swalaah, mtapata ujira wa Swalaah kama mko katika Swalaah mpaka mtakapotoka msikitini. Kuunganisha vidole wakati wa Swalaah ni kinyume na adabu ya Swalaah, basi mtu hatakiwi kuunganisha vidole wakati wa kusubiri Swalaah).’”

Soma Zaidi »

Mapenzi ya Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) wanaondoka kufanya hijrah usiku. Wakati wa safari, muda mwingine Abu Bakr Siddeeq alitembea mbele ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na kuna muda mwingine akitembea nyuma yake. Kuna wakati fulani alitembea upande wa kulia wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) …

Soma Zaidi »

Salaa na Salaam Tano za Imaam Shaafi’ee (rahimahullah)

Imetajwa kwamba baada ya kufariki Imaam Shaafi’ee (rahimahullah), mtu fulani alimuona katika ndoto na akamuuliza sababu ya kusamehewa na Allah Ta'ala. Imaam Shaafi’iee (rahimahullah) akajibu, “Ni kwa sababu ya salaa na salaam hizi tano juu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kuzisoma kila usiku wa ijumaa (yaani usiku unaotangulia Ijumaa).

Soma Zaidi »

Sunna za Msikiti

21. Usipite mbele ya mtu anayeswali. Lakini, ikiwa ameweka sutrah mbele yake (yaani kuweka kitu chochote kirefu ili watu wapite mbele yake), inajuzu kupita mbele ya sutrah.[1] عن أبي جهيم رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم لو يعلم المار بين يدي المصلي ماذا عليه لكان …

Soma Zaidi »

Mtu Kunywa kutoka Kwenye Howdh ul Kawthar ya Mustafa (sallallahu alaihi wasallam) na kikombe cha kipimo kamili.

Hasan Basri (rahimahullah) ametaja, “Yoyote anayetaka kunywa kutoka kwenye Howdh ul Kawthar (Sehemu Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) atawapa watu maji kunywa Siku ya Qiyaamah) ya Mustafa (sallallahu ‘alaihi wasallam) na kikombe cha kipimo kamili, basi amswalie Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kwa maneno yafuatayo: اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَعَلٰى آلِهِ وَأَصْحَابِهِ …

Soma Zaidi »

Sunna za Msikiti

18. Ni bora mtu asiutumie msikiti kama njia ya kupita (kupitia ng’ambo).[1] عن ابن عمر رضي الله عنهما عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال خصال لا تنبغي في المسجد لا يتخذ طريقا ولا يشهر فيه سلاح (سنن ابن ماجة، الرقم: 748)[2] Sayyidina Ibnu Umar (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Sayyidina …

Soma Zaidi »

Mapenzi Kwa Maswahaabah

Ja’far As Saaigh (Rahimahullah) anasimulia tukio hili ifuatayo: Miongoni mwa majirani wa Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahullah) alikuwa mtu ambaye alihusika katika madhambi mengi, maovu na vitendo visivyo na haya. Siku moja mtu huyu alikuja kwenye mkusanyiko wa Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahullah) na akamsalimia kwa salaam. Ingawa Imaam Ahmad …

Soma Zaidi »

Tafseer Ya Surah Al-Qaar’iah

Siku ya tukio la Mpigiko; na ni siku gani ya tukio la Mpigiko? Na nini kitakujulisha kuhusiana na tukio la Mpigiko? Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa. Basi ambaye mizani yake (ya amali) ni nzito, atakuwa katika maisha ya furaha. Na ama yule ambaye mizani yake ni nyepesi, makazi yake yatakuwa “Haawiyah” (shimo la Jahannam). Na nini kitacho kujulisha nini hiyo? (Ni) moto mkali.

 

Soma Zaidi »

Kutuma Salaa na Salaam juu ya Manabii (alayhi mus salaam) Wengine Pamoja na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah sallallahu alaihi wasallam alisema, “Jibreel (alayhis salaam) ametoka kwangu sasa hivi. Amekuja kunifahamisha kwamba Allah ta'ala amesema, ‘Hakuna Muislamu duniani anayetuma salaa na salaam juu yako (yaani juu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)) mara moja, isipokuwa kwamba Mimi na Malaika Wangu tutamtumia salaa na salaam juu yake (yaani nammiminia rehema kumi na Malaika wangu wamwombee msamaha mara kumi) kwa hivyo niswalie mara nyingi siku ya ijumaa, na utakapo niswalia, basi tuma salamu kwa Manabii (alayhi mus salaam), kwa sababu mimi ni Nabii miongoni mwa Manabii (alayhi mus salaam).”

Soma Zaidi »