Kuacha kitendo kinachompeleka mtu Jannah.

عن حسين بن علي رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من ذكرت عنده فخطىء الصلاة علي خطىء طريق الجنة (المعجم الكبير للطبراني، الرقم: 2887، وقال المناوي في فيض القدير (2/232) تحت حديث من نسي الصلاة علي خطئ طريق الجنة: لكن انتصر له ابن الملقن فقال: حديث ضعيف لكنه تقوى بما رواه الطبراني عن الحسن بن علي مرفوعا: من ذكرت عنده فخطئ الصلاة علي خطئ طريق الجنة، وتبعه الحافظ ابن حجر فقال: خرجه ابن ماجه عن ابن عباس والبيهقي في الشعب عن أبي هريرة والطبراني عن الحسين بن علي قال: وهذه الطرق يشد بعضها بعضا)

Sayyidina Husain Bin Ali (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “yule ambaye jina langu limetajwa na asinitumie salaam, atakuwa ameacha kitendo kinachompeleka Jannah.”

Kuandika salaat na salaam kwa namna ya kipekee

Sayyidina Abu Ali, Hasan Bin Ali At-taar (rahimahullah) anasema:

Abu taahir (rahimahullah) aliwahi kunipa maandishi machache ya Hadith. Niliona humo kwamba kila linapotajwa jina la Nabii wa Allah subhaana wata’ala, Maandishi ya Kumswalia Nabii wa Allah subhaana wata’ala yalikuwa yameadikwa kwa maneno haya:

صَلّٰى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَسْلِيْمًا كَثِيْرًا كَثِيْرًا كَثِيْرًا

Kisha nikamuuliza Abu Taahir, “Kwa nini unaandika salaa na salaam kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa namna hii?”

akajibu:

katika ujana wangu nilikuwa nikiandika hadith na sikuandika salaat kwa jina la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) basi nilimwona Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika ndoto na kumsalimia, lakini Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akageuza uso wake wa baraka kutoka kwangu. Kisha nilikuja kwake kutoka upande wa pili na kumsalimu tena, lakini kwa mara nyingine tena akageuza uso wake wa baraka kutoka kwangu. Kwa mara nyingine tena, kwa mara ya tatu. Nilimsogelea kutoka mbele na kumuuliza, “Ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), kwa nini unanigeuzia uso wako wa baraka?” .Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu, “‘sababu ni kwamba kila unapoandika jina langu katika kitaab chako, huniswalii”. Tangu wakati huo imekuwa ni kawaida yangu kwamba kila ninapoandika jina la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) naandika pia:

صَلّٰى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَسْلِيْمًا كَثِيْرًا كَثِيْرًا كَثِيْرًا

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …