Madhambi yatakuwa yamefutwa

عن أبي بردة بن نيار رضي الله عنه قال قال رسول الله صلي الله عليه وسلم من صلى علي من أمتي صلاة مخلصا من قلبه صلى الله عليه بها عشر صلوات ورفعه بها عشر درجات وكتب له بها عشر حسنات ومحا عنه عشر سيئات (السنن الكبرى للنسائى، الرقم: 9809، ورواته ثقات كما في فتح الباري 11/167)

Abu Burdah (radhiyallahu ‘anhu) Anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Kasema, “yoyote kutoka kwa ummah wangu anayetuma salaam moja juu yangu kutoka moyoni mwake wa dhati, Allah subhaana wata’ala atambariki na rehema kumi, atainua daraja lake aakhera kwa daraja kumi, ataandika matendo mazuri kumi kwa niaba yake na atafuta dhambi zake kumi .

Al Qawlul Badee

Allaamah Sakhaawi (rahimahullah) anasema:

Mwanafunzi wa kuaminika sana kutoka miongoni mwa wanafunzi wa Sheikh Raslaan (rahimahullah) aliniambia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alionekana katika ndoto yake na kitaab ‘AL Qawlul Badee’ (maelezo ya kitaab kuhusu kumswalia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) iliyoandikwa na Allaamah Sakhaawi (rahimahullah) ililetwa kwake, na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Alikubali.

Hii ilinifurahisha sana, na ninatumaini kuwa Allah subhaana wata’ala na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) wataikubali, na kwamba nitatuzwa sana katika ulimwengu huu na aakhera. Kwa hivyo nawasihi nyinyi nyote muendelee kusoma salaat juu ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Kwa dhati kabisa, kwa hakika swala yenu inamfikia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika kaburi lake la baraka, na majina yenu yanatajwa mbele yake.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …