CREATOR: gd-jpeg v1.0 (using IJG JPEG v62), quality = 85

Nyakati ambazo miswaak inapaswa kutumiwa

5. Meno yanapobadilika rangi au harufu mbaya hutoka mdomoni.[1]

عن جعفر بن أبي طالب رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال ما لي أراكم تدخلون علي قلحا استاكوا ولولا أن أشق على أمتي لأمرتهم أن يستاكوا عند كل صلاة (كتاب الآثار، الرقم: ٤١)

Imeripotiwa kutoka kwa Sayyidina ja’far (radhiallahu anhu) Kwamba wakati mmoja, sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alihutubia watu fulani akisema, “kuna nini mpaka nyie mnakuja kwangu katika hali ambayo naona meno yenu kuwa ni ya njano? Na Nimewashauri kusafisha meno yenu na miswaak.” Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kisha akasema, “kama isingekuwa hofu ya umma wangu kupata shida, hakika ningewaamuru (na kuilazimisha) watumie miswaak wakati wa kila salaa (hata hivyo, kutumia miswaak sio lazima lakini ni sunnah iliyosisitizwa wakati wa wudhu)”.

عن عبد الله بن بشر المازني رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم قصوا أظافيركم وادفنوا قلاماتكم ونقوا براجمكم ونظفوا لثاتكم من الطعام وتسننوا ولا تدخلوا علي قخرا بخرا (نوادر الأصول تحت الأصل التاسع والعشرين في باب النظافة)[2]

Sayyidina Abdullah Bin Bishr (radhiallahu anhu) Anaripoti kwamba sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, “punguza kucha zenu na mzike kucha zenu, safisha viungo vyenu vizuri, hakikisha fizi zenu zipo safi kutoka kwa masaliyo ya chakula, fanya miswaak, na usinijie ukiwa na hali ya kwamba nitakuta meno yenu kuwa ya njano na kutoa harufu mbaya.

6. Kabla na baada ya kula.[3]

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال إن كان قاله لولا أن أشق على أمتي لأمرتهم بالسواك مع الوضوء وقال أبو هريرة رضي الله عنه لقد كنت أستن قبل أن أنام وبعد ما أستيقظ وقبل ما آكل وبعد ما آكل حين سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول ما قال (مسند أحمد، الرقم: ٩١٩٤)[4]

Sayyidina Abu Hurairah (radhiallahu anhu) Anaripoti kwamba sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, na kwa hakika amesema, “kama isingekuwa hofu ya umma wangu kupata shida, ningewaamuru (na kuifanya iwe lazima kwao) kutumia miswaak wakati wa kila wudhu (hata hivyo, kutumia miswaak sio lazima lakini ni sunnah iliyo sisitizwa). ” sayyidina Abu Hurairah (radhiallahu anhu) Alisema zaidi, “kwa sababu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Kusisitiza utumiaji wa miswaak, nilifanya iwe tabia yangu kutumia miswaak kabla ya kulala, wakati wa kuamka, kabla ya kula na baada ya kula.”


[1] ويتأكد استحبابه في أحوال … وعند اصفرار الأسنان وإن لم يتغير الفم وعند تغير الفم بنوم أو طول سكوت أو ترك أكل أو أكل ما له رائحة كريهة أو غير ذلك (روضة الطالبين ١/١٦٧)

[2] قال صاحب نوادر الأصول وقوله لا تدخلوا علي قخرا بخرا المحفوظ عندي قلحا وقحلا والأقلح الذي اصفرت أسنانه حتى بخرت من باطنها ولا نعرف القخر والبخر إلا الذي نجد له رائحة منكرة يقال رجل أبخر ورجال بخر

[3] (ويسن للصلاة) … وللأكل (مغني المحتاج 1/166)

[4] قال الهيثمي: رواه أحمد ورجاله ثقات (مجمع الزوائد، الرقم: 1119)

About admin

Check Also

Njia ya sunnah ya kutumia miswaak Sehemu Ya Pili

1. Njia ya kushika miswaak ni kwa mtu kuweka kidole gumba chake na kidole kidogo …