9. Ni Mustahab kwa wale wanaokusudia kuchinja kutokukata kucha zao wala kukata nywele zao kwanzia mwanzo wa mwezi wa Dhul Hijjah hadi mnyama achinjwe.
Ummu Salamah (Radhiyallahu anha) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Yule anayekusudia kuchinja anapaswa aache kukata nywele zake na kukata kucha zake tangu mwezi wa dhul hijjah hadi baada ya kuchinja mnyama wake.
10. Takbeer-ut-Tashreeq inapaswa isomwe na wanaume na wanawake kutoka fajr ya 9 ya Dhul Hijjah hadi asr ya tarehe 13 wa Dhul Hijjah. Wanaume wataisoma kwa sauti na wanawake wataisoma kwa sauti ya chini baada ya kila swalaah ya fardh. Takbeer ya Tashreeq ni ifuatavyo:
اَللهُ أَكْبَرْ اَللهُ أَكْبَرْ لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ اَللهُ أَكْبَرْ اَللهُ أَكْبَرْ وَلِلّٰهِ الْحَمْدْ
Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) ni mkubwa zaidi! Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) ni mkubwa zaidi! Hakuna anayestahili kuabudu mbali na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala). Mwenyezi Mungu ni mkubwa zaidi! Mwenyezi Mungu ni mkubwa zaidi, na kwake peke yake ndiye sifa zote!
Imeripotiwa kutoka kwa Ali (Radhiyallahu anhu) kwamba alikuwa akisoma Takbeer-ut-Tashreeq kwanzia Salaah ya alfajiri siku ya Arafah (9 Zul Hijjah) hadi Salaah ya asr ya siku ya mwisho ya Tashreeq (13 Zul Hijjah).
11. Zidisha kumdhukuru Allah Ta’ala ifuatayo katika hizi Siku:
سُبْحَانَ اللهِ اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ اَللهُ أَكْبَرْ
Ibnu abbaas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Hakuna siku ndani ya mwaka ambao ibada ya Mwenyezi Mungu ni kubwa (katika thawabu) na mpendwa zaidi kwake yeye kuliko siku kumi za kwanza za Dhul Hijjah. Kwa hivyo, zidisheni kusoma Tasbeeh, Tahleel, Tahmeed na Takbeer. ” yaani سُبْحَانَ اللهِ اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ اَللهُ أَكْبَرْ