Katika hadith, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) ameelezea Ummah sifa za kibinadamu za Dajjaal. Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) akielezea kuhusu Dajjaal na sifa za mwili za kibinadamu zinaonyesha kwa ukweli kwamba Dajjaal pia ni mwanadamu. Kwa hivyo, imani ya Ahlus Sunnah Wal Jamaa ni kwamba Dajjaal ni mwanadamu, na ataibuka ulimwenguni kwa wakati maalum kabla ya Qiyaamah kama fitna kubwa kwa Ummah.
Hapo chini kuna sifa kumi za mwili, za kibinadamu za Dajjaal ambazo zimetajwa katika Ahaadith:
Kipengele Cha Kwanza: Dajjaal Kuwa Na Nywele za Singa
Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Usiku mmoja, nilijiona (katika ndoto) kwenye Ka’bah. Kisha nikamuona mtu aliye na rangi nyeupe kama ngano, ambaye alikuwa mtu mzuri zaidi ya mtu mwenye rangi ya ngano. Nywele zake zilikuwa kati ya masikio yake na mabega yake. Alikuwa amezitana, kwa hivyo zilikuwa zikiteleza na maji. Alikuwa akiegemea mabega ya watu wawili na kufanya Tawaaf ya Ka’bah. Niliuliza, ‘Mtu huyu ni nani?’ Niliambiwa, ‘Huyu ndiye Maseeh bin Maryam (‘ Alaihis Salaam). ‘Baadaye, nikamuona mtu fupi aliye na nywele za singa. Jicho lake la kulia lilikuwa na kasoro, kama zabibu inayojitokeza. Niliuliza, ‘Mtu huyu ni nani?’ Niliambiwa, ‘Huyu ni Maseeh, Dajjal.’ ”(Sahih Muslim #169)
Kipengele cha pili: Dajjaal kuwa na macho yenye kasoro
Macho yote mawili ya Dajjaal yatakuwa na kasoro. Lakini, jicho moja litafunikwa kabisa na ngozi, wakati jicho lingine litatoka na kufanana na zabibu (kama ilivyoelezwa kwenye hadith hapo juu).
Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Kwa kweli najua mambo yenye yapo pamoja na Dajjaal. Atakuwa na mito miwili inayotiririka. Mto Mmoja itaonekana wazi kuwa maji safi, wakati nyingine itaonekana kuwa moto mkali. Ikiwa mtu yoyote yuko wakati huo, kwa kweli anapaswa kwenda kwenye mto ambao anaona ni moto na kujiingiza ndani yake. Halafu, anapaswa ainamize kichwa chake na kunywa kutoka kutoka hyo maji, kwa maana ni maji baridi. Hakika, jicho la Dajjaal limefunikwa, juu yake ni ngozi nene. Imeandikwa kati ya macho yake neno ‘kafir’ ambalo kila muamini ataweza kuisoma, iwe anajua kusoma au hajuwi kusoma. ” (Sahih Muslim #2934)
Kipengele cha Tatu: Dajjaal kuwa mfupi, lakini mzito na mkubwa kimwili
Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Kwa kweli, Maseeh Dajjaal, ni mtu mfupi, visigino vyake viko mbali na miguu yake ikidumkizia ndani, nywele zake ni laini sana, moja ya jicho lake lina kasoro na nyingine imefutwa, sio ya kutoka au ya kudumkizwa. Ikiwa jambo linakusumbua, basi ujue kuwa Mola wako hana jicho lenye kasoro. ” (Sunan Abu Dawood #4320)
Katika Hadith nyingine, Tameem Daari (Radhiyallahu ‘Anhu), alimuelezea Dajjaal akisema, “Halafu, ghafla, ndani yake (kwenye kisiwa hicho) alikuwa mwanadamu mkubwa kabisa ajawahi kuona.” (Saheeh Muslim #2942)
Kipengele cha Nne: Miguu ya Dajjaal inayodumkiza ndani (yaani visigino vyake viko mbali na sehemu za mbele za miguu yake ziko karibu)
Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Kwa kweli, Maseeh Dajjaal, ni mtu mfupi, visigino vyake viko mbali na miguu yake ikidumkizwa ndani.” (Sunan Abu Dawood #4320)
Kipengele cha tano: Dajjaal kuwa na nywele nyingi na nene
Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Jicho la kushoto la Dajjaal litakuwa na kasoro na nywele zake zitakuwa nyingi na nene. Pamoja naye kutakuwa na bustani na moto. Kwa kweli moto wake ni bustani, na bustani yake ni moto.” (Saheeh Muslim #2934)
Kipengele cha Sita: Dajjaal kuwa na paji pana
Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Kuhusu Maseeh wa upotovu, ni mtu ambaye paji la uso wake ni pana, jicho lake la kushoto limefutwa na sehemu ya chini ya shingo lake ni pana. Yupo kama Abdul Uzza bin Qatan.” (Majma’uz Zawaa’id #12539)