Mtu Kuona Makazi Yake Peponi

عن أنس بن مالك قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى علي في يوم الجمعة ألف مرة لم يمت حتى يرى مقعده من الجنة (أخرجه ابن شاهين بسند ضعيف كذا في القول البديع صـ ٣٩٧)

Sayyidina Anas (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, “anaye soma salaamu kwangu mara elfu moja kwa siku ya ijumaa hata kufa mpaka aonyeshwe nafasi yake katika peponi.”

Tukio la Abu Imraan Waasity (rahimahullah)

Abu Imraan Waasity (rahimahullah) anaripoti:

Wakati fulani, nilikuwa katika safari ya kuelekea Madinah Tayyibah, wakati njiani, nilihisi kiu kali sana mpaka nilihofia maisha yangu. Kwa kuogopa kifo hicho kilikuwa karibu kunipata, nilikaa chini ya mti wa miiba.

Ghafla mpanda farasi akatokea mbele yangu juu ya farasi ya kijani, na hatamu za kijani na tandiko la kijani. Mkononi mwake alikuwa na kikombe cha kijani na kinywaji cha rangi ya kijani. Nilikunywa mara tatu kwenye hicho kikombe na hakuna ata tonye lililopungua kutoka kwenye hicho kikombe. Kisha akaniuliza naenda wapi, nikamjibu kuwa naelekea Madinah Munawwarah ili nimfikishie Salaam zangu kwa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na Maswahabah wake wawili.

Kisha akajibu, “Ukifika Madinah Munawwarah na ukawatolea salamu, basi nifikishie Salaam zangu vilevile kwa Nabi (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na maswahaba zake wawili. Waambie kwamba Ridwaan amefikisha Salaam zake. (Ridwaan ni Malaika ambaye ni mlinzi wa mlango wa Peponi).

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …