Mapenzi ya swahaba mmoja kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Swahaba mmoja siku moja alikuja kwa Nabii wa Allah sallallahu alaihi wasallam na kumuuliza, “Ewe! Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ni lini siku ya Qiyaamah?” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Umefanya maandalizi gani? kwa siku hiyo?” huyu swahaba akasema, “Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), sidai kuwa nina Swalaah nyingi, saumu na sadaqah nyingi upande wangu, lakini mimi nina mapenzi ya Allah subhaana wata’ala na Mtume Wake (sallallahu alaihi wasallam) moyoni mwangu.” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akasema: “Hakika kwenye Siku ya Qiyaamah, utakuwa pamoja na wale unaowapenda.”

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anasema, “Hakuna kilichowafanya Maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) kuwa na furaha zaidi kuliko maneno haya ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam).

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …