Sayyidina Abdullah bin Masood (radhiyallahu ‘anhu) ameripotiwa kusema: “Zilindeni Swalaah zenu tano za kila siku kwa kuzitekeleza mahali panapotolewa adhaan (yaani msikitini). Hakika kuswali hizi (Fardh) msikitini ni katika Sunan Huda (ibaadah zilizowekwa katika Dini). Allah Ta’ala ameamrisha Sunan Huda kwa ajili ya Nabii Wake (vitendo kama hivyo vya ibada ambayo ni uwongozi kamili kwenu). Wakati wa uhai wa Nabii (sallallahu alaihi wasallam) (Amna mtu alikuwa akiacha swalah ya jamaa msikitini isipokuwa mnafiki aliye wazi, kiasi kwamba hata mgonjwa alikuwa habaki nyumbani kuswali bali na kuswali Swalaah yake na jamaa msikitini na alikuwa akipelekwa msikitini huku akiwa ameungwa mkono kwenye mabega na watu wawili. Kila mmoja wenu (maswahaabah) ana sehemu maalum nyumbani kwake iliyotengwa kwa ajili ya kuswali nafl, n.k. Kwa Hivyo, ukianza kuswali fardh zako nyumbani na uondoki kuhudhuria Swalah ya jamaa msikitini, basi utakuwa unaiacha sunna iliyosisitizwa ya Nabii (sallallahu alaihi wasallam) Mara tu utakapoacha Sunna Mubaraka yake, hakika utapotoshwa.”
Imepokewa kwamba mtu fulani alimuuliza Sayyidina Abdullah bin Abbaas (radhiyallahu ‘anhuma), “Ni hali gani ya mtu anayefunga nafl mchana na akaswali nafl usiku mzima, lakini haendi msikitini kuswali na jamaa na kuhudhuria ijumah?” Sayyidina Abdullah bin Abbaas (radhiyallahu ‘anhuma) akajibu, “Amehukumiwa Motoni.”
[1] عن عبد الله بن مسعود قال حافظوا على هؤلاء الصلوات الخمس حيث ينادى بهن فإنهن من سنن الهدى وإن الله شرع لنبيه صلى الله عليه وسلم سنن الهدى ولقد رأيتنا وما يتخلف عنها إلا منافق بين النفاق ولقد رأيتنا وإن الرجل ليهادى بين الرجلين حتى يقام في الصف وما منكم من أحد إلا وله مسجد في بيته ولو صليتم في بيوتكم وتركتم مساجدكم تركتم سنة نبيكم صلى الله عليه وسلم ولو تركتم سنة نبيكم صلى الله عليه وسلم لكفرتم (سنن أبي داود، الرقم: 550)
[2] وسئل ابن عباس عن رجل يصوم النهار ويقوم الليل لا يشهد جمعة ولا جماعة فقال هو في النار (سنن الترمذي، الرقم: 218)