عن عبد الرحمن بن مريح الخولاني قال سمعت أبا قيس مولى عمرو بن العاص يقول: سمعت عبد الله بن عمرو يقول: من صلى على رسول الله صلى الله عليه وسلم صلاة صلى الله عليه وملائكته سبعين صلاة فليقل عبد من ذلك أو ليكثر (مسند أحمد، الرقم: ٦٦٠٥، وإسناده حسن وحكمه الرفع إذ لا مجال للإجتهاد فيه كما في القول البديع صـ ٢٣٧)
Sayyidina Abdullah Bin Amr Bin Aas (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti, “Yoyote atakaye tuma salaam kwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) mara moja Allah subhaana wata’alah na malaika wake watamtumia rehema na baraka sabini juu yake kwa kumlipa salaam yake moja. Kwahivyo yoyote atakaye taka kuzidisha kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) azidishe kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam). Na yoyote atakaye kuwa ataki kuzidisha kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) asizidishe kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) (yaani kama anataka kupata ujira mwingi,ni lazima azidishe kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam)).
Bilaal (radhiyallahu ‘anhu) Akiwa Kwenye kitanda chake cha kifo
Wakati Bilaal (radhiyallahu ‘anhu) alipokuwa karibu kuaga dunia, mke wake alianza kusema, “Ah, ni huzuni! Unaondoka katika ulimwengu huu.”
Bilaal (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Inapendeza na nifuraha kwamba kesho, tutakutana na marafiki zetu, tutakutana na Muhammad (sallallahu ‘alaihi wassallam) na maswahaba zake.”