1. Kufanya udhu nyumbani na kutembea kwenda msikitini kuswali ni njia ya mtu kusamehewa madhambi yake na daraja lake kuinuliwa.
Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kasema, “Mwenye kutawadha nyumbani na baada ya hapo kutembea kuelekea kwenye nyumba miongoni mwa nyumba za Allah (subhaana wata'ala) ili akamilishe faradhi ya Allah (subhaana wata'ala), Basi Kwa kila hatua moja anachukuwa, dhambi moja inasamehewa, na kwa hatua inayofuata, atainuliwa daraja moja."
Soma Zaidi »