Salamah bin Tammaam (rahimahullah) anasimulia:
Siku chache kabla ya Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) kufariki, mtu mmoja alikuja kukutana naye. Baada ya kukutana naye, yule mtu akamwambia, “Ewe Ibnu Mas’uud, jana usiku nilikuona katika ndoto. Katika ndoto, nilimwona Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akiwa amekaa juu ya mimbari na wewe ukiwa umekaa mbele yake chini.
“Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikuhutubia na akasema: ‘Ewe Ibnu Mas’uud, njoo kwangu, kwa sababu watu hawakukutendea mema (baada ya mimi kuondoka duniani).”
Ndoto hii ilikuwa ni dalili kwamba wakati wa Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuondoka hapa duniani ulikuwa umekaribia.
Baada ya mtu huyo kutaja ndoto hiyo kwa Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamuuliza: “Wallahi hivi kweli uliniona kwenye ndoto jana usiku?” Mtu huyo akajibu, “Ndiyo, niliona ndoto hii jana usiku.”
Baada ya hayo, Abdullah bin Mas‘uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia yule mtu: “Nakuomba ubaki Madinah Munawwarah kwa muda na uondoke tu Madinah Munawwarah baada ya kushiriki katika Swalaah yangu ya Janazah.”
Siku chache baadaye, Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alifariki na Swalaah yake ya Janaazah ikaswaliwa Madinah Munawwarah. (Usdul Ghaabah 285/3)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu