Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 7

26. Ni adabu kwamba mtu anapotembea na mwingine amekaa, basi anayetembea aanze kutoa salamu wa kwanza. Vile vile, wakati mtu mmoja anapopanda mnyama na mtu mwingine anatembea, basi yule ambaye kampanda mnyama aanze kutoa salamu wa kwanza. Na hivyo, vijana wanapaswa kuwasalimia wazee kwanza, na kikundi kidogo (wale ambao ni wachache kwa idadi) wanapaswa kusalimia kundi kubwa zaidi (wale ambao ni wengi) kwanza.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kumpanda mnyama amsalimie yule anayetembea kwanza. Anayetembea amsalimie aliyekaa kwanza. Wale walio wachache kwa idadi (kikundi kidogo) wanapaswa kusalimia walio wengi (kundi kubwa) kwanza. Vijana wanapaswa kuwasalimia wazee kwanza.”[1]

Kumbuka: Ingawa adabu ya Kiislamu ni kwamba makundi haya yaliyotajwa katika Hadithi yanatakiwa kusalimia kwanza, lakini kila moja anapaswa kujitahidi kutoa salamu kwanza, kwani ilikuwa ni sunna ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kusalimia kwanza mnapokutana.

27. Mtu hatakiwi kumtolea salaam asiye Mwislamu. Kama mtu asiye Muislamu akamsalimia muislamu kwa salaam, basi ajibu kwa kusema tu “Wa ‘alaik” (na juu yako), na ikiwa wengi wasio Waislamu wakamtolea salamu, mtu ajibu kwa kusema “Wa ‘alaikum” (na juu yenu nyote).[2]


[1] صحيح مسلم، الرقم: 2703

[2] عن أنس بن مالك أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: إذا سلم عليكم أهل الكتاب فقولوا وعليكم (صحسح مسلم، الرقم: 2163)

About admin

Check Also

Dua Baada Ya Kula 1

Dua ya kwanza: Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alitupa chakula na vinywaji na kutufanya Waislamu.

Dua ya pili Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alinipa chakula hiki kula, na alinipa bila juhudi yoyote au jitihada kutoka upande wangu.

Maelezo: Mu'aadh bin Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, "Yoyote anayekula chakula chochote na baada ya hapo anasoma Dua iliyotajwa hapo juu, dhambi zake zilizopita na za baadaye (ndogo) zitasamehewa. "