Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) Akiuonyesha Ummah Nafasi Tukufu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) wakati fulani alikua amekaa pamoja na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu), Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu), Abu Ubaidah (Radhiyallahu ‘anhu) na Maswahaba wengineo (Radhiyallahu ‘anhum) na kinywaji kikaletwa kwa Nabi (Sallallahu alaihi wasallam).

Nabi (Sallallahu alaihi wasallam) alichukua kinywaji hicho mkononi mwake na akampa Abu Ubaidah (Radhiyallahu ‘anhu) anywe kwanza. Lakini, Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu), kwa kumheshimu Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), hakutaka kunywa kwanza na akamwambia Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), “Ewe Rasulullah! Unastahili zaidi kunywa kwanza.”

Kisha Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akamwambia, “Abu Ubaidah, wewe kunywa (kwanza).” Abu Ubaidah (Radhiyallahu ‘anhu) kisha akakikubali chombo hicho kutoka kwa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).

Hata hivyo, kabla ya kunywa, kwa mara nyingine tena, kwa heshima na upendo kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), akamwambia Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), “Ewe Rasulullah! Chukuwa wewe (na kunywa kwanza).” Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akamwambia:

اشرب فإن البركة مع أكابرنا

“(Ewe Abu Ubaidah!) wewe kunywa (kwanza), kwa sababu barakah ziko kwa wazee wetu (yaani umma utapata baraka kutoka kwa Allah Ta’ala kwa kuwaonyesha heshima wazee wao na kuwaruhusu kufanya mambo kwanza).”

Baada ya hapo Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema:

من لم يرحم صغيرنا ويجل كبيرنا فليس منا

“Mtu asiyewaonea huruma vijana miongoni mwetu na hawaheshimu wakubwa miongoni mwetu, basi yeye si miongoni mwetu (yaani hafuati njia yetu – njia ya sunna).”

(Majma’uz Zawaaid #8264)

Maelezo: Inapaswa ikumbukwe kwamba wakati wa kuwa na wazee wetu, sunnah ni kwamba mtu aonyeshe upendo na heshima kwao. Dalili ya kuonyesha upendo na heshima kwao ni kwamba mtu huwapa upendeleo kuliko yeye mwenyewe.

Ni kwa ajili hiyo ambapo Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) – imamu wa Manabi na Marasul wote – alipompa kinywaji Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ili anywe kwanza, hakutaka kunywa kwanza, lakini mara mbili alimuomba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) anywe kabla yake, kwani Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) ndiye anayestahiki zaidi kunywa kwanza.

Hata hivyo, pale Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alipomuamrisha kunywa kwanza, kisha akasalimu amri, kwa sababu kutii amri ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) (au mkubwa wa mtu) kutapewa upendeleo kuliko hamu ya mtu kutaka kuonyesha heshima yake, na hii itawafikiana na sunna katika hali hii.

Kutokana na tukio hili, tunaona kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alitaka kuuonyesha ummah nafasi ya juu na utukufu wa Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ili nao wamheshimu ipasavyo.

Njia moja ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kuwaonyesha Maswahabah (na Ummah) Nafasi tukufu ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ilikuwa ni kuwaeleza kwa maneno wema. Haya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) ameyafanya kwa kuwambia umma kwamba Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) ndiye muaminifu wa umma huu.

Njia ya pili kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kuwaonyesha Maswahabah (na Ummah) nafasi tukufu ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ilikuwa ni kuonyesha vitendo mbele yao ili waelewe heshima na nafasi yake na hivyo pia kumuonyesha heshima. Kwa hiyo, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alimuomba kunywa kwanza – kuonyesha ummah nafasi yake tukufu na heshima.

About admin

Check Also

Shemeji Wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam)

Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alioa wake wanne. Kila mmoja katika wake zake wanne alikuwa dada …