Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 6

18. Ukiingia kwenye mkusanyiko wenye mazungumzo au majadiliano ya Dini inafanyika, hupaswi kutoa salaam kwa sababu hili litamsumbua mwenye kuongea pamoja na wale waliohudhuria mkusanyiko huo.

19. Ikiwa mtu amezama katika mazungumzo au anajihusisha na baadhi ya mambo basi ni bora mtu asimsalimie. Lakini, ikiwa mtu anajua kwamba hatokuwa na tatizo nalo basi mtu anaweza kumsalimia.

20. Haijuzu (makrooh tahreem) kupiga magoti na kutoa salaam.

21. Wakati unajisaidia, hupaswi kutoa salaam kwa mtu yoyote au kujibu salamu ya mtu yoyote. Vile vile, ikiwa mtu anajisaidia, hupaswi kumtolea salamu.

22. Unapaswa kutoa salaam kwa wazee wako kwa unyenyekevu kwa sauti ya chini.

23. Ukiahidi kufikisha salaam ya mtu kwa mtu, inakuwa ni wajibu kwako kutimiza ahadi na kufikisha salamu.

24. Sunnah ya salaam haipo kwa watu wazima tu. Wakati unapokutana na watoto, mtu anapaswa pia kuwasalimia kwa salaam. Wakati Nabii (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa akiwaona watoto, alikuwa akiwatolea salamu.[1]

25. Mnapokutana, mnapaswa kuanza mazungumzo yenu na salaam.

Jaabir (radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Salamu itolewe kabla ya mazungumzo.”[2]


[1] صحيح مسلم، الرقم: 2168

[2] سنن الترمذي، الرقم: 2699، وإسناد ضعيف لضعف محمد بن زاذان كما في إتحاف الخيرة المهرة 4/281

About admin