Qataadah (rahimahullah) anasimulia kwamba Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akisema, (kwa khofu ya kusimama mbele ya Allah Ta’ala Siku ya Qiyaamah na kutoa hesabu ya matendo yake):
وددت أني كنت كبشا، فيذبحني أهلي، فيأكلون لحمي، ويحسون مرقي.
“Jinsi ninavyotamani ningekuwa kondoo tu. Wamiliki wangu wangenichinja, kula nyama yangu na kunywa mchuzi wangu.” (Siyaru Aa’laamin Nubalaa 3/14)
Kwa maneno mengine, khofu ya Allah Ta’ala na kulazimika kutoa hesabu ya matendo yake ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba alitamani angekuwa kondoo tuu ili asitoe hesabu ya matendo yake huko Akhera.