Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 5

13. Unapotoka nyumbani, toka nyumbani na salamu.

Qataadah (radhiyallahu anhu) ameripoti kuwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mkiingia nyumbani, basi wapeni salamu waliomo ndani yake, na unapotoka (nyumbani), basi acha salamu yako kama amana kwa watu wa nyumbani kwako (yaani salamu kwa watu unapoondoka).”[1]

Maelezo: Nabii (sallallahu alaihi wasallam) ametufundisha kutoa salaam wakati wa kuondoka nyumbani na akasema, “Acha salaamu yako kama amana kwa watu wa nyumbani kwako”. Kwa ujumla, mtu anapoweka amana na mtu fulani, anarudi baadaye kuipokea. Kwa hivyo, mtu anapoacha amana ya watu wa nyumbani kwake, ni kama mtu anaota ishara nzuri na kuweka matumaini yake katika rehma za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah), kwamba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) atamrudisha kwake.

14. Mwenye kutoa salaam kwanza anapata malipo makubwa zaidi.

Imepokewa kutoka kwa Abu Umaamah (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kuwasalimia watu wakwanza kwa salamu ndiye aliye karibu zaidi na Allah Ta‘ala (yaani yupo karibu zaidi na rehma za AllahTa’ala).[2]

15. Mtu anapokufikishia salamu ya mtu kwako, basi unapaswa kujibu kwa kusema “Alaikum wa alaihimus salaam”. Lakini, ikiwa mtu atajibu kwa kusema tu “Wa alaikumus salaam”, itatosha.

16. Ni wajibu kujibu salamu iliyoandikwa katika barua/SMS/email n.k. Jibu linaweza kutolewa kwa maandishi au kwa maneno.

17. Si sahihi kuandika salaam kwa njia ya mkato yaani kwa kifupi. (k.m. slmz, salaams, n.k.). Hii haiendani na heshima ya salaam. Ikiwa salaam iliandikwa kwa njia ya mkato (k.m. slmz, salaams, n.k.), haitakuwa waajib kuijibu.


[1] عن قتادة قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: إذا دخلتم بيتا فسلموا على أهله فإذا خرجتم فأودعوا أهله بسلام (شعب الإيمان للبيهقي، الرقم: 8459، هكذا جاء مرسلا وسنده جيد كما في التيسيير للمناوي ١/٩٤)

[2] سنن أبي داود، الرقم: 5199، وسكت عنه هو والمنذري في مختصره

About admin

Check Also

Fadhila za Jumu’ah

Kusamehewa Madhambi Kwa Kuswali Jumu’ah Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu …