Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 4

11. Ikiwa kikundi cha watu kinakutana na mtu mmoja, na mmoja kati ya kundi anatoa salaam, basi salaam yake mmoja itatosha kwa niaba ya kundi nzima. Vile vile mtu akikutana na kundi la watu na kuwasalimia, jibu la mtu mmoja kutoka katika kundi litatosha kwa niaba ya watu wote kwenye kundi.

Ali (radhiyallahu anhu) anasema kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Wakati kundi la watu linapopita karibu na mtu, basi itawatosheleza wote kama mmoja wao akitoa salamu (kwa mtu wanayekutana naye), na kundi la watu linapoketi, basi inawatosheleza wote ikiwa mmoja wao atajibu salamu (kwa mtu anayewasalimia kwa salamu).

12. Toa salaam unapoingia nyumbani. Ikiwa hakuna mtu nyumbani, unapaswa kutoa salamu kwa kusema:

اَلسَّلَامُ عَلَيْنَا وَعَلٰى عِبَادِ اللهِ الصَّالِحِيْنَ

Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah).[2]

Anas (Radhiyallahu anhu) anasema: Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) siku moja aliniambia, “Ewe mwanangu kipenzi, unapoingia nyumbani kwako, wasalimie ahli zako (yaani watu wa nyumbani) kwa salaam. Hii itakuwa njia ya kupata baraka kwako na kwa familia yako.”[3]


[1]سنن أبي داود، الرقم: 5212، وقال الحافظ في الفتح 11/7: واحتج للجمهور بحديث علي رفعه يجزئ عن الجماعة إذا مروا أن يسلم أحدهم ويجزي عن الجلوس أن يرد أحدهم أخرجه أبو داود والبزار وفي سنده ضعف لكن له شاهد من حديث الحسن بن علي عند الطبراني وفي سنده مقال وآخر مرسل في الموطأ عن زيد بن أسلم

[2] عن ابن عمر في الرجل يدخل في البيت أو في المسجد ليس فيه أحد قال: يقول: السلام علينا وعلى عباد الله الصالحين (المصنف لابن أبي شيبة، الرقم: 26353، وسنده حسن كما في فتح الباري 11/ 20)

[3] سنن الترمذي، الرقم: 2698، وقال: هذا حديث حسن غريب

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 1

1. Unapokutana na ndugu yako Muislamu, muamkie kwa kutoa salaam. Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaripoti …