Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani Saa’idah (bustani ya matunda ya Bani Saa’idah) kumchagua Khaleefah mpia kutoka miongoni mwao.

Wakati huo, Abu Bakr na Umar (radhiyallahu anhuma) walikuwa nyumbani kwa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) na walikuwa hawajui kinachoendelea. Wakiwa nyumbani, Umar (radhiyallahu anhu) ghafla akasikia sauti ikiita kutoka nje ikisema, “Ewe mtoto wa Khattaab! Toka, (kwa sababu nataka nijadili mambo nawewe)!” Lakini, Umar (radhiyallahu anhu) alijibu, “Ondoka kwa kuwa nina shughuli nyingi sasa (wakati huo, mwili uliobarikiwa wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) ulikuwa bado nyumbani kwake na ulikuwa bado haujazikwa)!”

Sauti kisha ikasema, “Njoo nje, kwani jambo kubwa linakaribia kutokea. Ma answaar wamekusanyika ili wamchague kiongozi miongoni mwao, basi nendeni kwao kabla haijatokea suala na vita kutokea baina yenu na wao.”

Kusikia hivyo, Abu Bakr na Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) mara moja wakaondoka nyumbani kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na kuelekea kwa thaqifah Banu Saa’idah. Wakiwa njiani, walikutana na Abu Ubaidah bin Jarraah (radhiyallahu anhu), ambaye pia alifuatana nao.

Baada ya kufika Thaqifah Bani Sa’diah, mazungumzo marefu yalifuata baina ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) na ma answaar. Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwaeleza kwamba alimsikia Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akitaja kwamba Khaleefah anaweza tu kuchaguliwa kutoka kwa Maquraish na kwa vile hawakuwa Maquraishi, Khalifah hawezi kutoka kwao.

Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) kisha akawaambia ma answaar huku akiwa ameshika mikono ya Umar na Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhuma), “Napendelea mchague yoyote kati ya hawa wawili (kuwa khaleefah wa Waislamu, basi chagua mtakayemtaka).”
(Musnad Ahmad #391)

Wakati huo, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwahutubia ma answaar na akasema: “Enyi watu wa Ansaar! Je, hujui kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amemuamuru Abu Bakr kuwaongoza watu katika Swalaah? Ni nani kati yenu basi atakuwa na ujasiri wa kusimama mbele ya Abu Bakr (na kuongoza Swalah kama Khalifa)?” Kusikia hivyo, Ma answaar wakasema, “Tunajikinga kwa Allah Ta’ala ili tusimame mbele ya Abu Bakr!”

Baada ya hapo, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alishika mkono wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kuweka kiapo cha utii kwake, akifuatiwa na Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) na kisha Answaar. Baada ya hapo, Maswahaba wengine wote pia waliweka kiapo cha utii kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu).

Kutokana na tukio hili, tunaona msimamo mkubwa wa Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu), kwamba Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipendekeza kwamba awe ndiye Khaleefah wa kwanza wa Uislamu.

Hata hivyo, Maswahabah wote (Radhiya Allaahu ‘anhum), akiwemo Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) hawakukubali pendekezo hili, na wote walikubaliana kuwa hakuna Sahaabi ambaye ni mkubwa kuliko Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) na yeye ndiye anaestahiki zaidi ukhalifa.

About admin

Check Also

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) Akiuonyesha Ummah Nafasi Tukufu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) wakati fulani alikua amekaa pamoja na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu), …