28. Waislamu wawili wanapokutana, basi baada ya kutoa salamu, wafanye musaafahah (wapeane mikono).
Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “(Wanapokutana Waislamu wawili basi) ukamilisho wa maamkiano yao ni kwamba wafanye musaafahah wao kwa wao.”[1]
29. Wakati wa kufanya musaafaha ni sunna kufanya musaafahah kwa mikono miwili.
30. Unapofanya musaafahah, shikilia tu mkono wa mwingine. Hakuna haja ya kutingisha mikono, kama wanavyofanya na kafiri. Vile vile, baada ya kufanya musaafaha, mtu hatakiwi kubusu mkono wake mwenyewe na kuusugua kwenye kifua chake kwa sababu tendo hili hayana msingi katika Dini.
31. Unapofanya musaafahah, usimfinye mikono kwa nguvu kiasi kwamba unamsababishia maumivu au ugumu.
32. Usifanye haraka kuondoa mikono yako baada ya kufanya musaafahah. Badala yake, unapaswa kuruhusu mtu mwingine aondoe mkono wake kwanza.
Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba wakati mtu yoyote angekutana na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na kufanya Musaafahah, alikuwa haondoi mkono wake mpaka yule mtu mwingine auondoe mkono wake kwanza, na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa ageuzi uso wake (kuondoka mahali ya mkutano) mpaka yule mtu mwingine augeuze uso wake kwanza (kuondoka mahali ya mkutano).[2]
[1] سنن الترمذي، الرقم: 2730، وقال الحافظ في الفتح 11/56: وقد أخرج الترمذي من حديث بن مسعود رفعه من تمام التحية الأخذ باليد وفي سنده ضعف وحكى الترمذي عن البخاري أنه رجح أنه موقوف على عبد الرحمن بن يزيد النخعي أحد التابعين
[2] سنن الترمذي، الرقم: 2490، وقال: هذا حديث غريب