Talhah (radhiyallahu anhu) katika Vita vya Uhud

Zubair bin Awwaam (radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba katika tukio la Uhud, Mtume (sallallahu alaihi wasallam) alivaa vazi la kivita mara mbili.

Wakati wa vita, Mtume (sallallahu alaihi wasallam) alikusudia kupanda juu ya jabali lakini kutokana na uzito wa zile vazi mbili, hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo alimwomba Talhah (radhiyallahu anhu) aketi ili aweze kuchukua msaada kutoka kwake na kupanda kwenye jabali. Talhah (radhiyallahu anhu) mara moja aliketi chini na kumsaidia Mtume (sallallahu alaihi wasallam) kupanda juu ya jabali.

Zubair (radhiyallahu anhu) anasema kwamba alimsikia Mtume Muhammad (Sallallahu alaihi wasallam) akisema wakati huo, “Imekuwa ni waajib kwa Talhah (yaani Jannah imekuwa waajib kwa Talhah).”

Katika vita vya Uhud, Talhah (radhiyallahu anhu) kwa ushujaa alifuatana na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na akamlinda. Wakati wowote Maswahaba (radhiyallahu anhum) walipojadili vita vya Uhud, walikuwa wakisema kwamba siku hii (siku ya Uhud) ilikuwa ya Talhah (radhiyallahu anhu). Talha (radhiyallahu anhu) alikuwa amemkinga Mtume (sallallahu alaihi wasallam) na mwili wake. Alipata majeraha zaidi ya themanini kwenye mwili wake, lakini hakuacha upande wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), ingawa mkono wake ulikuwa umepooza kutokana na majeraha makali.

About admin

Check Also

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) Akiuonyesha Ummah Nafasi Tukufu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) wakati fulani alikua amekaa pamoja na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu), …