Jumu’ah

Siku ya Jumu’ah ina umuhimu mkubwa katika Uislamu. Ni miongoni mwa neema kubwa za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) juu ya ummah huu ni sifa adhimu ya Uislamu.

Amesema Mtume (sallallahu alaihi wasallam):

“Siku ya Jumu’ah ni sayyidul ayyaam (yaani kiongozi wa siku zote na ni siku kubwa zaidi (kuliko siku zingine ndani ya wiki) mbele ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah). Ni fadhila kubwa kuliko siku ya Eid Ul Adha na siku ya Eid Ul Fitr mbele ya Allah Ta’ala.

“Kuna matukio matano maalum ambayo ni makhususi kwa siku ya Jumu’ah. (Kwanza,) katika siku hii, Allah Ta‘ala alimuumba Nabii Aadam (alayhis salaam). (Pili,) Allah Ta’ala alimtuma Nabii Aadam (alayhis salaam (na Hawaa alayhas salaam) duniani katika siku hii. (Tatu,) siku hii, Nabii Aadam (alayhis salaam) alifariki (na akarudishwa kwenye makazi yake ya asili). (Nne,) katika siku ya Jumu’ah, kuna muda maalum (wa kukubaliwa) ambapo dua yoyote atakayomba mja kwa Allah Ta’ala, itajibiwa dua yake, maadamu haombi kitu chochote cha haramu. (Tano,) siku hii Qiyaamah itatokea.

“Hakuna Malaika aliye karibu na Allaah, wala mbingu wala ardhi, wala mlima au bahari, isipokuwa anaiogopa Siku ya Jumu’ah (kwa sababu ya kuwa Qiyaamah kitatokea siku hii).”

Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) ametaja kuwa siku ya Jumu’ah ni siku yenye mwanga, na usiku wa Jumu’ah ni usiku yenye nuru.

Katika Hadith, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ameuusia Ummah kuzidisha salaa na salaam juu yake siku ya Jumu’ah, kwa sababu hii itakuwa ni sababu ya msamaha wao na njia ya kupata dua zake.

Umar bin Khattaab (radhiyallahu anhu) anasimulia kwamba Mtume (sallallahu alaihi wasallam) alisema: “zidisheni kunitumia salaa na salaam katika usiku na mchana wa Jumu’ah kwa sababu salaam zenu zinaletwa kwangu. Kisha nakuombeeni dua kwa Allah Ta’ala na kumuomba akusameheni madhambi yenu.”

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 5

13. Unapotoka nyumbani, toka nyumbani na salamu. Qataadah (radhiyallahu anhu) ameripoti kuwa Rasulullah (sallallahu alaihi …