Yearly Archives: 2022

Sunna Za Msikiti

33. Kama unasinzia msikitini basi badili sehemu yako kwa kusogea na kukaa sehemu tofauti msikitini, ilimradi sio wakati ambapo khutba inaendelea. Kupitia kuhamia mahali pengine, usingizi wa mtu huondolewa.[1] عن ابن عمر رضي الله عنهما قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول إذا نعس أحدكم وهو في المسجد …

Soma Zaidi »

Mapenzi ya ‘Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam)

Usiku ule Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) anatoka kwenda kuhijiria kwenda Madinah Munawwarah, makafiri walikuwa wameizunguka nyumba yake ili wamuue. Kabla ya kuondoka, Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alimuagiza ‘Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) kulala nyumbani kwake ili makafiri wafikirie kuwa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) bado yuko ndani na hawatatambua kuwa alikuwa ameondoka. …

Soma Zaidi »

Tafseer Ya Surah Takaathur

Kushindana baina ya watu katika kukusanya mali (na manufaa ya dunia) kumekushughulisha (kutoka katika utiifu wa Allah Ta‘ala na Akhera). (Hili linaendelea) mpaka mtazuru makaburi (yaani mpaka mtakapofariki). Hapana! hivi karibuni mtakuja kujua (ukweli wa mambo ya dunia ukilinganisha na Akhera, na malengo ya kweli ambayo mlipaswa kuyapigania). Tena, hivi karibuni mtakuja kujua (ukweli). Hapana! Lau mngelijua kwa ujuzi wa yakini (basi msingefanya hivi). Bila ya shaka mtaliona Moto wa Jahannam. Kisha bila ya shaka mtaliona kwa jicho la yakini. Kisha bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo (Siku ya Qiyaamah), kuhusu neema zote (mlizozistarehesha duniani).

Soma Zaidi »

Sunna Za Msikiti

31. Mbali na kwenda msikitini kuswali, ikiwa kuna shughuli inayofanyika msikitini, basi mtu aweke nia ya kwenda msikitini kupata elimu ya Dini. Ikiwa mtu ana uwezo wa kufundisha Dini basi afanye nia ya kuja msikitini ili kuwapa watu elimu ya Dini ikiwa atapata fursa ya kufanya hivyo.

Soma Zaidi »

Mapenzi ya Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Katika tukiyo la Hudaybiyah, Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameamrishwa na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kujadiliana na Maquraishi huko Makka Mukarramah. Wakati Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameondoka kwenda Makka Mukarramah, baadhi ya Maswahaba walimwonea wivu Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kwa kuweza kufanya tawaaf ya Nyumba ya Allah subhaana wata’ala Kwa upande mwingine, …

Soma Zaidi »

Kupata Rehma Kumi

Sayyiduna Abu Huraira (radhiyallahu 'anhu) ameripoti kuwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema " yoyote atakaye nitumia salaam mara moja, allah subhaana wata'alah atamtumia salaam (yaani atampa zawadi na atamfariji na rehema zake) kwake mara kumi" 

Soma Zaidi »

Sunna Za Msikiti

27. Uwe mtulivu na mwenye heshima ukiwa msikitini, wala usighafilike na kusahau heshima ya msikiti. Baadhi ya watu, wakiwa wanangoja Swalah ianze, wanahangaika na mavazi yao au wanacheza na simu zao za mkononi. Hii ni kinyume na heshima na adabu ya Msikiti.[1] 28. Kusaidia katika usafi wa msikiti.[2]  عن أبي …

Soma Zaidi »

Mapenzi ya Umar (radhiyallahu ‘anhu) na Kumbukumbu za Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Usiku mmoja, katika kipindi cha ukhalifa wake, Umar (radhiyallahu ‘anhu), alikuwa kwenye ulinzi wa usalama na aliona mwanga na kusikia sauti ikitoka katika nyumba fulani. Alimkuta bibi kizee ndani yake akisokota pamba na kuimba nyimbo zifuatazo: عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَاةُ الْأَبْرَارْ ** صَلَّى عَلَيْكَ الْمُصْطَفَوْنَ الْأَخْيَارْ “Wacha Mungu waendelee kutuma salamu …

Soma Zaidi »

Bashara Nzuri Kutoka Kwa Allah( Subhaana Wata’alah) Kwa Wale Ambao Wanamsalia Mtume

عن عبد الرحمن بن عوف رضي الله عنه قال خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم فاتبعته حتى دخل نخلا فسجد فأطال السجود حتى خفت أو خشيت أن يكون الله قد توفاه أو قبضه قال فجئت أنظر فرفع رأسه فقال ما لك يا عبد الرحمن قال فذكرت ذلك له فقال …

Soma Zaidi »

Sunna za Msikiti

25. Usipasue vifundo vyako ukiwa msikitini. Vile vile, usiunganishe vidole vyako ukiwa umeketi msikitini.

Mtumwa aliyeachiliwa huru wa Sayyidina Abu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) anasema, “Siku moja, nikiwa na Abu Sa’eedd (radhiyallahu ‘anhu) na yeye akiwa pamoja na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), tuliingia msikitini na tukamuona mtu mmoja ameketi katikati ya musjid. Mtu huyu alikuwa amekaa kitako kwa jinsi magoti yake yalivyoinuliwa, na mikono yake ikiwa imezunguka magoti yake, na vidole vya mikono yake yote miwili vimeunganishwa. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliimpa ishara mtu huyu (kuvuta mazingatio yake), lakini mtu huyo hakuona ishara ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam). Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hivyo akageuka kumelekea Abu Sa’eed (radhiyallahu ‘anhu) na akasema, ‘Mmoja wenu atakapokuwa msikitini, basi asiunganishe vidole vyake, kwani kuunganisha vidole vyake ni kutoka kwa Shetani. Kwa muda utabakia msikitini mkingojea Swalaah, mtapata ujira wa Swalaah kama mko katika Swalaah mpaka mtakapotoka msikitini. Kuunganisha vidole wakati wa Swalaah ni kinyume na adabu ya Swalaah, basi mtu hatakiwi kuunganisha vidole wakati wa kusubiri Swalaah).’”

Soma Zaidi »